Msanii Kali P hataki tena kusikia muziki

Msanii Kali P hataki tena kusikia muziki

Nani ana video ya mzee yusuph wakati anaaga kuacha muziki 🤣🤣🤣
Aliaga kwa mbwembweee haram sheikh mziki haram.....kapigwa njaa hata mwezi haujaisha karudi kutuburudisha.
Ngoja nsikilize kwanza kibao chake hapa V. I. P huwa kinankumbusha mbali chuo huko nikiwa namiliki sabufa babu.
 
Hebu hukooo.....aliaga mzee yusuph, amezungukwa na masheikh anabubujikwa michozi, yuko wapi leo. Njaa ni kitu kingine
Mzee Yusufu alijua akiimba Kaswida angeoiga hela, kwahiyo na hao masheikh walio mzunguka walikuwa wajanja wajanja, ndio maana ikawa rahisi kurudi.

Wapo ambao Nia zao zilikuwa njema na Allah akawafanyia wepesi wakabaki katika msimamo na hawakurudi na hawatorudi.

Mziki ni Ushetani kama akili yako inakuwa nafanya kazi vizuri uhitaji kuambiwa.
 
Kula tende sheikh kula tende
 
Wasanii wa zamani wengi wamevurugwa wana stress sana.

Mb dogg nipo nae kitaa ubungo makuburi.. haeleweki yaani
Kila nikipita nyuma ya roman catholic namuona pale kwenye matairi Ile nyumba karibu na msikiti yani michongo inaonekana imebuma kbsa
 
Mbona nilishawahi kusikia eti anafanya biashara ya vinyango huwa ana export nchi za Germany, Holland na UK ?

Hizo biashara nyingine zipo midomoni mwa watu tu, Ujerumani, Uholanzi na UK watu hawana habari ya kununua vinyago. Wakija Bongo wananunua kama souvenirs na bei ni rahisi
 
Msanii aliyetamba na ngoma ya Imekaa vibaya na Tumbo joto , Abdul Miraj maarufu kama Kali P amesema hataki tena kusikia masuala ya Muziki .

Kali P amesema ameamua Kumrudia Muumba wake na sasa hive ana takribani miaka 12 ameingia katika dini na ameachana na maswala ya Muziki.

"katika dini yetu ya Uislamu muziki ni haramu ndio maana mimi nikajitoa kwa sababu ya kumuogopa Mungu, Kama Ujumbe kuna njia watu kuwafikishia ila sio Mziki, siku ambayo niliacha mziki nafsi yangu ilisema sipendi tena Mziki. Kipindi nafanya Muziki nilikuwa na miaka 22, nyimbo zangu zikipigwa najisikia vibaya sana na sina habari nazo tena, atakayeimba atakuwa anajichochea moto mwenyewe" Alisema Kali P

kali P kwa sasa anafahamika kama Sheikh Abdul Miraj na anapatikana maeneo ya Kitunda.
Ni kweli Mziki zamani ulikua haulipi, watu walifanya mziki kama starehe na njia yakufungua fursa nyingine.
 
Muziki wa zamani haukuwa na hela ndio maana wanauchukia.

Internet na Digital platforms ndio zimeleta utajiri kwenye muziki. Leo hii ray vanny anapewa ubalozi wa tembo card crdb na kukunja milioni 500. Anaanzia wapi kuuchukia mziki.

Huwezi msikia alikiba aseme anauchukia mziki.. huku ameimba toka enzi za kina Kali P wanaimba
Toa sifuri moja hapo, afu inayobaki igawe kwa 1.5

Ni kweli muziki zamani haukuwa na hela. Lakini hata leo muziki bado hauna hela.

"Muziki hauna hela, nilizotarajia kuzipata" youngkiller msodoki.
 
Hana tofauti na mzee Yusuph. Alisema amemrudia Mungu kumbe aliona upepo umeisha. Baada ya muda kidogo akarudi tena na hapo ndipo alipotezwa mazima.

Ifike mahali msanii akiwa na heshima mtaani aitumie vizuri. Ukiona umeanza kuchuja unatangaza kustaafu na sio kumrudia Mungu. Hii itafanya usikose vimiamia vya shows za birthday parties na watu wataendelea kusikiliza nyimbo zako zilizohit huku wakiacha kukusumbua na ngoma mpya. Utakuwa legend
 
Kuna yule wa Daz Nundaz anaitwa Sajo naye Kuna siku nilimuona maeneo ya Kimara Korogwe yupo na kimashine Cha Kubetisha Cha Premier Bet. Yaani kachoka na Kawa kama kapagawa 😭😭😭
Haha Sajo AkA mentali..
Dah umenikumbusha mbali snaa
 
Hana tofauti na mzee Yusuph. Alisema amemrudia Mungu kumbe aliona upepo umeisha. Baada ya muda kidogo akarudi tena na hapo ndipo alipotezwa mazima.

Ifike mahali msanii akiwa na heshima mtaani aitumie vizuri. Ukiona umeanza kuchuja unatangaza kustaafu na sio kumrudia Mungu. Hii itafanya usikose vimiamia vya shows za birthday parties na watu wataendelea kusikiliza nyimbo zako zilizohit huku wakiacha kukusumbua na ngoma mpya. Utakuwa legend
Wapo wanaoacha kweli kama suma lee
 
Wapo wanaoacha kweli kama suma lee
Mmoja kati ya 10.

Na wengine miongoni mwa wanaoacha kweli, wanakuwa wamepata channel ya kuwaingizia kipato.

My brother usijaribu kuweka agano na masikini wa fedha, akipata mwenye fedha atasahau agano lako na yeye. Anaweza hata kukuangamiza.

Yuda aliangalia mkoba wenye fedha akajua Yesu akifa, (yuda) atakiliki zile fedha.
 
Hallow P Funky, hebu nikopeshe buku japo nipate tumbaku, naona aibu sana! Sijui kesho nitaamka mapema
 
Sasa muziki wake ulikua hauna matusi wala pombe shida au uharamu wake ni nini...
 
Back
Top Bottom