Msanii Madee unatuumiza na kututia hasira mno sisi Hustlers

Msanii Madee unatuumiza na kututia hasira mno sisi Hustlers

Kwa kauli hiyo. Kesho magazeti ya udaku yatakuwa na vichwa vya habari kama hivi " madee achoma gari yake" ha ha ha ha nasubiri kwa hamu kesho kusikua madee kachoma gari kisa kipondo cha 1-0
 
Madee limbukeni tu na ni kwa sabab kashika hela kias ukubwani..angekua na hela kama za wanamuziki wanigeria sijui angesemaje... Achome tu hata akitaka avute ule moshi wakati anachoma...ila akumbuke hajafika hata Mr. Nice alikokua amefika...na amuulize
 
Namshauri Madee, kulikoni alichome hilo Gari ni Bora akalitoa Msaada kwenye Hospitali likatumika Kubebea Wagonjwa. Au akalipeleka Moja kwa moja kwenye serikali yake ya Mtaa huko manzese anakoishi na kulikabidhi huko ili lisaidie kubebea wamama wajawazito wanao patwa na Uchungu Usiku wa Manane.

Kwa kufanya hivyo anaweza akapata heshima kubwa sana ndani ya Jamii inayo mzunguka.

By the way Timu yake Imeshindwa tayari. Hivyo namsihi abadiishe fikra zake.
Mkuu huyu Madee ni maskini wa akili... Atakua kakulia uswazi ambako hawawazi...huko ndo kunakuaga na ushabiki wa aina yake...
 
Haya ndo baadhi ya mambo aliyosema mgombea urais wa Marekani wa sasa mzungu Donald Trump kuhusu watu weusi watu wakapiga kelele sana
 
Mziki wa madee nay wa mitego na kitale au mkude simba na mafanikio yao haviendani kabisa
Muziki ni kazi iliyokufanya umfahamu Madee, llakini Madee hategemei muziki peke yake.
 
Kusema team yangu ikifungwa nitachoma moto gari yangu ni dalili ya ulimbukeni na uasikini wa fikra tu, mtu mwenye pesa hawezi kuweka Nadhiri ya kipuuzi kiasi hicho.
 
nataka nione Moshi wa gari lililochomwa unavyo kuwa....teh teh chezea Chelsea..?!
 
Ilo gari si akampe baba yake kibaha Maili Moja anatembea kwa miguu tu mzee wa watu" mtoto hana adabu huyu kwa uwezo gani aliokua nao achome gari.
Au kuna ngoma anataka kutoa /kiki
 
Hivi Inaingia Akilini Kwenu Mtu Ambaye Anajua Fika Kuwa 90% Ya Watanzania Ni MASIKINI Wa KUTUKUKA Ambao Kila Siku Tunahangaika Kuutafuta Mkate Na Sometimes Tunalala Tu " Kavu Kavu " Na Kupiga " Miayo " Huku Tukikodolea Mikenchi Tu Majumbani Kwetu Halafu Msanii Mmoja Wa Bongo Fleva Madee Anakuambia Kuwa Endapo Timu Yake Ya Arsenal FC Leo Itafungwa Na Chelsea FC Ktk LONDON DERBY Basi Atachoma Moto Moja Ya Gari Lake La Kifahari. Na Ikumbukwe Kuwa Madee Hana " CHOMBO CHA USAFIRI " Nikimaanisha Zile Gari Zenye Thamani Ya Kati Ya Tsh Milioni 3 Hadi Tsha Milioni 15 Ambazo WATANZANIA Wengi MNAZO Bali Madee Ana " MAGARI " Nikimaanisha Kuwa Magari Yake Mengi Yanaanzia Tsh Milioni 50 Hadi Tsh Milioni 120.


Naomba Kuuliza Je Hii " Nadhiri " Aliyoiweka Madee Ya Kuchoma Moto Moja Ya GARI Zake Siyo Ni TUSI LILILOTUKUKA Kwa Sisi " MANGUMBARU? " a.k.a Masikini? Kweli Kuna Watu Wana NYODO, KASHFA Na MATUSI Ya Reja Reja Hapa Duniani. Kwanini Tu Asingeliweka Kama BAHATI Nasibu Hilo Gari Lake Ili Akina Siye TUPAMBANE Kuligombania Na Tulipate Kwani Kusema Ukweli TUMESHACHOKA SASA KUOTA VIGIMBI VYA KUKIMBILIA MADALADALA, KUPIGWA NDOLE NA KUIBIWA Huku TUKIJAMBIWA KILA MARA NDANI YA VYOMBO VYA USAFIRI Kiasi Kwamba Ikifika Iwe Kazini au Nyumbani Unanuka SHOMBO Tu.


Tafadhali Kwa Aliye Karibu Na Msanii MADEE Naomba Amwambie Asilichome Moto Hilo GARI Lake Na Kama Vipi Alitafutie Tu UTARATIBU Sisi MANGUMBARU Tulipate Na Tutamshukuru Mno.
Kumbe na wewe unaandikaga pumba humu,rubbish
 
Mbaya sana..... Sometimes ushabiki huwa ni kama addiction ya cocaine, sasa kwa upande wake kama msanii na kioo cha jamii hajafanya jambo la hekma kutoa kauli ya kuchoma gari lake moto ukiangalia mpaka hapo alipo ni usanii ambao ni sisi mashabiki ndo tunamlipa kwa perfomance yake,pale anaposema anachoma gari lake actually hatupaswi kuwa wasemaji sana koz its his personal property but akitaka kingne sisi ndo atatualiki kwenye matamasha sasa ukiwaza wewe kama shabiki kuwa iyo pesa yaenda ku betiwa kwa kuchomwa....!? better than angeigawa kwa msaada kuliko kuchomwa daaaah anyway life goes on
 
Back
Top Bottom