Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,471
- 752
Staa kinda katika Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu' amefungua kinywa na kujibu skendo iliyoenea jijini Dar es Salaam kuwa, amehongwa gari na kigogo mmoja ambaye jina halikupatikana mara moja.
Akizungumza na Amani jijini Dar juzi, Lulu aliyefanya ‘wandaz' kwenye Filamu ya Tatuu alifunguka kuwa, suala la yeye kuhongwa gari aina ya Toyota Starlet ambalo linachukua kasi mithili ya moto wa kifuu kitaani, halina ukweli kwani anaendesha magari mengi.
Alisema: "Jamani nachukizwa na watu wanaofanya kazi ya kupakazia wenzao. Kwanza kabisa sikumbuki ni lini niliendesha Starlet kwa sababu huwa nasukuma mikoko ya aina tofauti tena mikali.
"Hiyo ni skendo tu wameamua kunipikia. Ukweli mimi sina na wala sijahongwa gari, sema tu huwa natumia magari ya kukodisha kwa watu tofauti tofauti.
"Kwanza mtu akisema kuna mwanaume amenihonga gari hata siwezi kujua ni nani kwa sababu natumia magari ya watu wengi kwenye mizunguko yangu."
Katika sura nyingine, Lulu aliwashangaa wanaosema kahongwa Starlet, gari analoamini kuwa siyo la kupewa yeye kwa hadhi yake.
"Ha! Starlet, yaani ndiyo gari la ‘saizi' yangu? Si kweli, mimi naendesha magari makali na siyo la aina hiyo."
Hata hivyo, Lulu alimalizia kwa kuwataka mastaa wenzake kuacha majungu na kuweka juhudi katika kazi zao za sanaa.