Msanii mpya wa WCB (Zuchu) ni sifuri

Msanii mpya wa WCB (Zuchu) ni sifuri

KiponzaOne

Member
Joined
Dec 3, 2018
Posts
6
Reaction score
36
Diamond ametuletea msanii gani? Yani haka kasichana kanakoitwa Zuchu kweli ndio kaje kushindana kwenye hili soko lenye waimbaji mahiri wa kike kama Nandy, Ruby, Maua Sama, Vanessa, Jide na wakali wengine wa kike wa hapa bongo? Kweli? Kwa sauti ile? Pengine kwa kuwa ni mtoto wa yule mama ndio maana Diamond amemsaini. Lakini kuimba anajua kidogo sana na muziki anaotunga hauwezi kufika popote. Hakuna cha maana walichofanya wasafi.

Hata Jolie, Karen, Winnie wana sauti kumzidi. Diamond hukuona wote hawa? Au waligomea kujiunga na wewe? Mihela unaiteketeza bure kwa huyu msichana.

Ila nahisi kama naanza kujishangaa mwenyewe kwa kuandika yote niliyoandika hapo juu. Nakumbuka mwaka 2015 wakati Harmonize anatambulishwa na wimbo wake wa kwanza nilitoa maoni yanayofanana na hayo kuhusu huyo Zuchu. Nilisema kuwa Harmonize asingefika kokote. Hana kipaji chochote zaidi ya kumuiga Diamond. Mshamba asie na swaga zozote. Akatoa ngoma kama Bado, Nambie, Kwangwaru na nyingine nyingi ambazo zilifanya vizuri mno. Bado nikamponda sana.

Lakini eti leo napaza sauti mbele ya watu kuwa Harmonize anajua kuliko Diamond. Najiita 'Team Konde Boy'. Mimi ni mnafiki sana. Yani kwa sababu Harmonize ametoka WCB eti leo najifanya kumsapoti. Najiuliza akirudi tena Usafini nitakuwa na maoni gani kuhusu muziki wake. Naomba asirudi. Nitakosa pa kuiweka sura yangu.

Dada Zuchu naomba usinisikilize. Nilimkandia hata Mbosso pia wakati anatambulishwa. Nilisema hawezi hata kukaribia levo za Aslay. Lakini leo hii muziki wake unasikilizwa zaidi kuliko wa Aslay. Nafuta kauli zangu zote hasi dhidi ya Zuchu. Ni chuki zangu tu dhidi ya Diamond ndio zimenifanya kuwa mnafiki. Nilikuwaga 'Team Kiba' sasa hivi najiita 'Team Konde Gang'.
 
Pale mtu anapotaka kulazimisha mtizamo wako uwe ni wa kila mtu,ila mwisho wa siku muda na number zitaongea.

Hata yule aliyeindoka kundini mwanzoni walidai kafanana na Mondi wakadai Mondi anapoteza mda na hela yake,baadaye wale waliomponda wanamkubali.
 
Natamani zuchu angejikita kwenye taarabu kama mama yake(khadija kopa)yaani ile taarabu hasa.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Natamani zuchu angejikita kwenye taarabu kama mama yake(khadija kopa)yaani ile taarabu hasa.
Ila baadae akiwa maarufu comment yako itabaki humuhumu usisahau hilo kipindi fulani harmonize alipondwa humu kwamba hana kipaji diamond anapoteza hela yake bure pia ana iga iga kila kitu kwa diamond kuanzia sauti, swaga mpaka Melody sasa Kiko wapi?Pia mbosso wakati anatambulishwa na WCB Kuna watu pia waliponda Kama wewe wanasema unamuacha aslay eti unamsajili mbosso ila leo hii tunazungumza mbosso amekuwa msanii mkubwa anayefanya vizuri kuliko aslay na watu wamemsahau huyo aslay waliokuwa wanamlilia.
 
Mleta uzi mimi nmekuelewa...sjui kwa nini wachangiaji wengine wanashindwa kukuelewa..

Uandishi mzuri sana huu..
 
Mke mwenza hadi wa leo harmo anapondwa na mmoja wa wapondaji ni wewe. Tuje kwa mbosso mmeshamfikisha kimataifa?mbona nyimbo zake ni za kudumu wiki moja tu?

Back
Top Bottom