KiponzaOne
Member
- Dec 3, 2018
- 6
- 36
Diamond ametuletea msanii gani? Yani haka kasichana kanakoitwa Zuchu kweli ndio kaje kushindana kwenye hili soko lenye waimbaji mahiri wa kike kama Nandy, Ruby, Maua Sama, Vanessa, Jide na wakali wengine wa kike wa hapa bongo? Kweli? Kwa sauti ile? Pengine kwa kuwa ni mtoto wa yule mama ndio maana Diamond amemsaini. Lakini kuimba anajua kidogo sana na muziki anaotunga hauwezi kufika popote. Hakuna cha maana walichofanya wasafi.
Hata Jolie, Karen, Winnie wana sauti kumzidi. Diamond hukuona wote hawa? Au waligomea kujiunga na wewe? Mihela unaiteketeza bure kwa huyu msichana.
Ila nahisi kama naanza kujishangaa mwenyewe kwa kuandika yote niliyoandika hapo juu. Nakumbuka mwaka 2015 wakati Harmonize anatambulishwa na wimbo wake wa kwanza nilitoa maoni yanayofanana na hayo kuhusu huyo Zuchu. Nilisema kuwa Harmonize asingefika kokote. Hana kipaji chochote zaidi ya kumuiga Diamond. Mshamba asie na swaga zozote. Akatoa ngoma kama Bado, Nambie, Kwangwaru na nyingine nyingi ambazo zilifanya vizuri mno. Bado nikamponda sana.
Lakini eti leo napaza sauti mbele ya watu kuwa Harmonize anajua kuliko Diamond. Najiita 'Team Konde Boy'. Mimi ni mnafiki sana. Yani kwa sababu Harmonize ametoka WCB eti leo najifanya kumsapoti. Najiuliza akirudi tena Usafini nitakuwa na maoni gani kuhusu muziki wake. Naomba asirudi. Nitakosa pa kuiweka sura yangu.
Dada Zuchu naomba usinisikilize. Nilimkandia hata Mbosso pia wakati anatambulishwa. Nilisema hawezi hata kukaribia levo za Aslay. Lakini leo hii muziki wake unasikilizwa zaidi kuliko wa Aslay. Nafuta kauli zangu zote hasi dhidi ya Zuchu. Ni chuki zangu tu dhidi ya Diamond ndio zimenifanya kuwa mnafiki. Nilikuwaga 'Team Kiba' sasa hivi najiita 'Team Konde Gang'.