Msanii msomi Nikki wa Pili na Fiesta

Mapensho star

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2016
Posts
3,052
Reaction score
4,104
Kijana ambaye pamoja na usomi wake na uwezo mkubwa wakuchambua mambo ya uchumi ameshaimba vibao vingi ambavyo kwa asilimia kubwa vinaamasisha vijana kufanya kazi na kuacha kuajiliwa leo hii yeye mwenyewe ananishangaza kupakiwa kwenye gari la fiesta kwa wale wanyonyaji.

Hivi yeyi mwenyewe hajijui kuwa anatumiwa na watu wasioenda shule?

Najua Nikki shule unayo kipaji unacho ya nini tena ubabaishwe ni kutojiamini tu navyoona wasanii mnashindwa na haka kabinti ka Ruby kamejitambua mapema!!

Ya nini mashabiki wakuone kila siku unazungushwa kila mkoa alafu hauna hata kiwanja ukirudi Dar hauna kitu?
 
Kwani we ulitakaje?asiende fiesta halaf hela ya mtaji wa kujiajiri ungempa wewe?au asiende fiesta kisa rubby hajaenda?...
 
Japo uwa simpendi kwa kujifanya anajua kila kitu ila napingana na mleta mada.
Tatizo hakuna mwenye hakika nikki na wenzake wanalipwa kiasi gani ni ushabiki tu.
Hata mbele wakiwa kwente tour wanatumiaga mabasi miji hado miji unless kama wanaenda umbali mrefu.
Sasa mlitaka wawapandishe ndege wakati kuna sehemu nchi hii fiesta inatimba lakini viwanja vya ndege hakuna.
Na jambo la kushangaza unakuta anayetoa ushauri hapa kaajiliwa kwa muhindi au serikalini anaamka saa 12 asubuhi kila siku kazini anasubiri aje apokee laki nane kwa mwezi, yeye kashindwa kujiajiri na kuona anavyo nyonywa lakini anamsema mwenzake.
 
ni msomi lakini ana njaa kali na hana ujanja wa kupiga pesa kwa kutumia usomi wake haina namna lazima apande costa na man fongo.
 
Huyo Nikki aliwafata kuwalilia shida? au ni kimbelembele chenu tu kutazama ya wenzenu na kufumbia macho ya kwenu?.

Ni wivu tu wa mafanikio ndio unaowasumbua juu ya huyo Nikki,hakuna kingine unachoweza sema zaidi ya hicho.

Ama kweli Nyani haoni kundule,vijana fanyeni kazi zenu acheni MAJUNGU na UMBEA mtandaoni.
 
Rubby hajui alitendalo.....
 
Sasa huyo ni msomi kijana yuko hivyo....... utamshangaaje Prof. Lipumba kung'ang'ania madaraka??? watanzania aliyeturoga alishakufa kitambo, tunayaishi tusiyoyazungumza na kuyazungumza tusiyoyaishi.......
 
Ajira ni ajira tu.ulipwenkwa mwezi,kwa siku kwa kazi kwa masaa au kwa mwaka .ye alisema mwenyewe hataki kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…