Wasanii wa HipHop kibongo bongo ni wabishi kwelikweli. Yaani unapoleta mambo za kumshauri afanye kitu kulingana na wakati unatakaje, anaona kama unamtoa kwenye reli na hivyo anakujibu kuonesha kuwa anachokifanya ndicho sahihi - JIWE type.
Mwaka 2015 niliwahi mwambia Nikki Mbishi aka Zohan kubadili muundo wa muziki wake na kuufanya kibiashara akaleta majibu kama hizo kuwa anafanya kwa wanaopenda na sio kwa wote. Ajabu, role model wao unakuta ni Dr. Dre ambaye sasa anafanya nyimbo za kuendana na wakati ila wao hawataki, wanakomaa na 'misingi', sishangai Nash Mc kukataa kuuza album kisasa, ni utaratibu wao 'ku-keep it real.'