Kagi Rasta
JF-Expert Member
- Oct 20, 2016
- 264
- 441
Leo mida ya sa11 na nusu jioni nilikua nasikiliza kipindi cha redio kwenye Metro FM ya jijini Mwanza ambapo msanii aliyetamba sana na kundi la wakali kwanza QJ alikuwa akihojiwa na akasema kwamba anarudi tena kwenye game ya mziki na kundi lao la Wakali Kwanza nalo linarudi huku akisema kwamba kaja Mwanza kimziki zaidi na kutoa nafasi kwa msanii yoyote ambaye yuko tayari kufanya nae kazi amtafute kwa namba zake au zile za mtangazaji wa redio.
QJ alitamba na nyimbo kama Sifai, Nimebaki lonely, Kitu gani & Natamani huku akisema anamkubali sana msanii Ben Pol.
Sasa Kinachoshangaza hapa ni kwamba QJ alitangaza kuachana na mziki wa bongo fleva na kujikita katika mziki wa injili na kumtumikia Mungu huku akisisiza hataki kukumbukia maisha ya mziki aliokuwa anaufanya zamani.
Sasa cha ajabu leo hii katangaza kurudi kwenye game huku akiwa kaishaandaa baadhi ya nyimbo.