Tetesi: Msanii Rashid Abdallah Makwiro 'Chid Benz' ajiunga katika lebo ya WCB

Tetesi: Msanii Rashid Abdallah Makwiro 'Chid Benz' ajiunga katika lebo ya WCB

lil wayne

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2016
Posts
992
Reaction score
904
Msanii maarufu wa miondoko ya kufoka/kurapu Rashid Abdallah Makwiro al maarufu kama CHID BENZ amejiunga rasmi katika lebo ya Wasafi Classic Baby WCB mchana Iliyo chini ya mwanamuziki machachari kabisa Diamond platnumz.

Taarifa hizi zimepatikana kupitia mtu wa karibu sana wa Babu Tale. Na pia kituo cha kuaminika cha redio yaani CloudsFM kimetaarifu mchana huu.
 
Nimeipenda hii...

Cha msingi asije akamvimbia rais au akamfunza kula na kuvuta yale madude...

Hivi diamond ameshaandaa sera za WCB?
 
Naona taratibu dogo Mondi ana transion kutoka kwenye u entertainer na kuelekea kwenye u music mogul.

Kwa kweli juhudi za huyo dogo nazipenda maana kaweza kujikwamua kutoka kwenye hali duni sana ya kimaisha hadi kufika hapo alipo.

#Positivity#
 
Kama hii habari ni ya kweli, basi WCB naipunguzia marks ya kufanikiwa kutoka 100 na kuwa 50/50.
 
WCB isije kuwa kama kokoro, linakusanya kila kitu, Kenge, Kaa, Samaki na kila kiumbe cha majini.

Katika kutaka kujitanua na kubeba wasanii wengi wanatakiwa kuchuja. siyo kila aina ya Msanii ni wakusajiliwa na Label hiyo. Nadhani mpaka kufikia hapa wameshajipapambanua ni lebal ya namna gani na wasanii wa aina gani.

Waangalie, kunawasanii wanaweza kuiangusha lebo yao kwa namna moja ama nyingine.

BACK TANGANYIKA
 
Mtoto akizaliwa ni ishara ya neema maana ukoo unaongezeka.
Sidhani kama ungeipongeza wcb ungepungukiwa na kitu maana wanastahili kupongezwa kwa kukuza wcb.
WCB IMEANZA CHUKUA WASANII WA CHINI YA KIWANGO
 
Back
Top Bottom