Msanii Ray C azidiwa na Madawa ya Kulevya; asaidiwa na Polisi

Atajioneaje huruma kama hajitambui? Tunaojitambua ndiyo tunapaswa kuwatambua na kuwasaidia wale waliokwisha kufikia hatua ya kutojitambua (waathirika). Na Ray C ni mmoja wa hao wanaohitaji msaada kutoka kwa wale wanaojitambua na pia kuwa tayari kusaidia.

Na pia watu wanamuonea huruma Ray C kwa vile ni mmoja wa wasanii waliopata majina makubwa nchini Tanzania na hivyo tutake tusitake kujulikana kwake na pia kumbukumbu nzuri ya muziki wake vichwani mwa washabiki wake zinamfanya apate sympathy kubwa kuliko watu wengine wengi tu wenye matatizo kama yake au pengine kupita hayo ya kwake.

Na nionavyo Ray C ni reference nzuri inayoweza kutumika kuwaonya watoto wetu majumbani na wengineo mitaani juu ya kuepuka madawa ya kulevya. Uzuri wa reference yake unatokana na kujulikana kwake katika jamii na akija kupona anaweza kuwa mmoja wa wahamishaji wazuri kwa vijana ili waepuke madawa ya kulevya na starehe zingine zisizo na tija katika maisha yao.
 
Nini kinachowashinda kujua kipi kibaya kipi kizuri kwa hawa wasanii wetu...karne hii kweli mtu hajui madhara ya cocaine?kujiendekeza tu.
 
Kama hiyo ni reference ya utumiaji wa hayo makitu yawezekana kuna jambo la kujifunza. Hebu tujifikirishe kidogo, mbona ni muda mrefu amekuwa akijishughulisha na kuwashawishi watu wasitumie hayo makitu au alikuwa anafanya kinyume chake?
 
...si vema kumhukumu, haswa sisi tunaoamini ktk Kristo huwa tunasamehe na kuombea. Angeweza kuokoka anaweza kupona kabisa.
we nae, hv unajua matatzo yakuombea watu, sasa unakula unga mpka yameenea kweny damu yote na yameharibu brain tena kwakujitaki. unaombea hapo mungu afanyeje sasa? atoe damu chafu yote au? acha kumpa Mungu vimajukumu vya kipuuzi.
 
Guys hivi stim za nyagi kweli hazitoshi..... !?? hapana.... hawa hata tone la huruma sitoi..
 
Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo,atavunjika ghafula wala hapati dawa Mithali 29:1.
 
Tulitumia fedha kumpeleka kutibiwa nje ya nchi na akarudi amepona ,shauri yake atamkumbuka sana mzee kikwete.Hakuna namna dunia itamfunza yeye ni mtu mzima sasa aendelee na madawa ya kulevya mwisho atauona.
 
Kijijini kwetu ni Masaki na sina ndugu wa kumlilia wote mambo yao ni mazuri.
daah nimesikia aibu kusoma coment yako,hauna akili hata moja aisee,sometimes ukikaa kimya inakuwa bora zaidi kuliko ku expose ujinga wako kwa halaiki,pole sana aisee..
 
Hivi kuna watu mnajua ni nini maana ya addiction ..

Watu wanashindwa kuacha ngono za michepuko seuze hizo dawa !!!!!....
HAKUNA KITU KIGUMU KAMA KUSHINDANA NA TAMAA YA NAFSI YAKO INAYOSABABISHWA NA HITAJI LA MWILI WAKO

Ray c siyo teja kama mateja wengineo....alikuwa ni mtu maarufu sana pembeni ya mwenzie jay dee.aliwaumbia mioyo ya kuthubutu mabinti wengi waliokuwa na ndoto za kuwa wanamuziki

Si ndugu yangu ila ni mtanzania mwenzangu..kuna haja gani ya kufurahia anguko lake ????...

HUU NI ZAIDI YA UCHAWI
 
Daah huyu mtu amechoka kweli,sijui tunamsaidiaje huyu, maana nilikuwa pale nilisikitika sanaa!
 
MASIKINI RAY C Kashindwa kuhimili presha za MAISHA sasa anatafuta shortcut.............daaaaah wamuache tu avute mpaka siku akiondoka DUNIANI jamani amechagua...au RAIS amfunge maana huyu raisi wetu ndio atamueza.
 
..kumhurumia huyu mtoto ni kumchimbia kaburi!
...."roho mbaya" tu ndo salama yake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…