Nyaka-One
JF-Expert Member
- Oct 27, 2013
- 4,730
- 6,736
Atajioneaje huruma kama hajitambui? Tunaojitambua ndiyo tunapaswa kuwatambua na kuwasaidia wale waliokwisha kufikia hatua ya kutojitambua (waathirika). Na Ray C ni mmoja wa hao wanaohitaji msaada kutoka kwa wale wanaojitambua na pia kuwa tayari kusaidia.Yeye mwenyewe anatakiwa kujitambua na kutambua njia za kushinda matatizo yake. Ni kweli mwenzetu ana matatizo na anahitaji huruma. Ingawa kama binaadamu twatakiwa kumuonea huruma mwenzetu, lakini kama yeye hataki kujionea huruma unafikiri wengine watawaza nini?
Na pia watu wanamuonea huruma Ray C kwa vile ni mmoja wa wasanii waliopata majina makubwa nchini Tanzania na hivyo tutake tusitake kujulikana kwake na pia kumbukumbu nzuri ya muziki wake vichwani mwa washabiki wake zinamfanya apate sympathy kubwa kuliko watu wengine wengi tu wenye matatizo kama yake au pengine kupita hayo ya kwake.
Na nionavyo Ray C ni reference nzuri inayoweza kutumika kuwaonya watoto wetu majumbani na wengineo mitaani juu ya kuepuka madawa ya kulevya. Uzuri wa reference yake unatokana na kujulikana kwake katika jamii na akija kupona anaweza kuwa mmoja wa wahamishaji wazuri kwa vijana ili waepuke madawa ya kulevya na starehe zingine zisizo na tija katika maisha yao.