Msanii Roma Mkatoliki amevuka mstari mwekundu lakini anachekewa tu!

Watu wenye mtazamo kama wewe ndiyo maana wanakufa kiboya sana
 
Sawa mchambuzi a.k.a chawa lialia
 
Roho yako mbaya,fasihi andishi hajataja jina la mtu wa msoga Wala wa ikulu ila wewe ni mchochezi
 
Wewe ni mlamba viatu a.k.a Praise team ya Lumumba (Lumumba buku 7)

Roma kaamu kugusa mshono naona unataka WATU WASIO JULIKANA WAMFUATE STATE (US)

Mama Samia ana moyo mpana hawezi kumchukia Roma au kumu angamiza kisa kumkosoa kwenye huu WIMBO.....

Kuna watu walimchongea yule Mwandishi MUHAYA Kwa wenye mamlaka akafundishwa adabu najua hawezi kusahau mpka kaburini........

Tuna Jenga nyumba Moja haina haja ya kugombea fito.........🤓🤓🤓🤓

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
Umeuelewa huo mstari vizuri au na wewe umeropoka? Au Kuna ukweli unaoujua ndiyo Maana unampinga Roma?
 
Mama kaudhibitishia ulimwengu kuwa anaweza sawa njoo kwenye uhalisia anavitu gani alivyovifanya vikubwa zaidi kuwazidi waliomtangulia mpaka sasa

Jitahidi utoke huko uliko Rais sio Mungu asisemwe rafiki yangu,au wewe ni miongoni wa wale watu wakiambiwa ukweli anasema umemtusi au kumdharau huo wimbo uko vizuri tena kwa wakati sahihi
Zama chimbo yaani chukua mstari mmoja mmoja alafu ufatilie utanishukuru mle ni ukweli
 
Yoga alidokeza KIDOGO kwenye dark days!!

Hawezi fungiwa coz katumwa aitoe HIYO na wakubwa!

Lengo ni kuchonganisha kambi hizo zenye maslahi yao na uongozi uliopo!!
 
Kwani uongo???Hata Magufuri alikuwa anaongoza kwa Remote ya Ali Hassan Mwinyi ili avurunde na kweli alivurunda na hata Mama Samiah atavurunda kweli kweli kama Kikwete ndiyo icon yake.
 
Dah wewe jamaa ni kilaza aiisee na utakuta ety ni baba wa familia kabisa??
 
roma ameuliza?

ni kama mayala alivyouliza kwenye makala sabufa povu likamtoka chamwino amedharau mhimili.

wewe sabufa mna tofauti gani?
 
Kelele za Mlango hazimfanyi mwenye Nyumba asilale ila akizisikiliza hatolala kweli.

Wanaopenda kwenda mbele ni wachache ila watakao kurudi wakawe makondoo ni wengi.

Shida ya waafrika usihangaike kuwapigania maana watakupiga wewe ili wapate haki ya kupigwa na mtesi wao.

Unafiki, unafiki ,unafiki ndio maisha ya Waafrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…