Msanii Roma Mkatoliki amevuka mstari mwekundu lakini anachekewa tu!

Msanii Roma Mkatoliki amevuka mstari mwekundu lakini anachekewa tu!

Ukweli kumdhihaki ,kumkedi na kumweka msambweni mh.Rais SSH kwa kumwita "mwendeshwa akili"?!!!

Huyu Ibra anadharau sana...
Huyu mpare wa Tanga ni mkorofi sana....ametuumiza sana kumtukana mama yake na mama yetu sote daaaah

#SiempreJMT[emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Mhhh kamtukana au kamwambia.
 
Nyimbo kama za Roma ndio zinatakiwa kuimbwa na wasanii karibu 90% kwa sababu Tanzania inahitaji ukombozi wa kifikra, kisiasa, kijamii na kiuchumi.
 
Wimbo wenyewe mm sijawahi usikiliza , hua nasikiliza nyimbo ili kutafuta burudani na kukonga nyoyo tu , ila nyimbo za kupigana vijembe hua sisikilizi kabisa

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Hujasikia pale aliposema yeye ni mmoja wa wanaomkubali mama au hapo hapakuhusu Mkuu.

Ila Roma muongo sana anasema yeye sio chadema wala ccm wakati alitangazwa alipopewa kadi ya chama 😂😂 au anafikiri tumesahau kuwa yeye ni bavicha 😂
 
Yote ni tisa. Kumi katika mistari ya Roma ambapo amevuka mstari mwekundu ni pale anaposema, "Mama (Samia) anaongoza yuko Ikulu lakini rimoti iko Msoga (Jakaya Kikwete).

Huku si tu Roma ametweza taasisi ya Rais lakini pia amemdharau na kumdhihaki Rais Samia Suluhu Hassan kwamba hawezi kuongoza hadi ashikiwe akili na Rais mstaafu Jakaya Kikwete jambo ambalo ni uzushi, uongo na upuuzi wa kisanii

Roma amevuka mpaka wapi? Maneno yote ya kwenye mistari hapo juu ni ya Kweli ; Kwani nani asiyejue kuwa Vasco Dagama ndio mshauri wake mkuu, hakuna appointment inafanyika bila endorsement toka Msoga!!
Enzi ya Magufuli ulikuwa unamsikia mkwere ? Alikuwa hana sauti na alikuwa amejichimbia Msoga lakini mara baada ya kumsimika Samia akarurudi Mjini fulltime; kule shamba anakwenda kutambika tu!!
Nyie machawa ndio mnatafsiri vibaya wimbo wa mzalendo ROMA!
 
Uhuru wa kujieleza haumaanishi kuvuka mipaka. Uhuru wako usivuke mipaka na kumkwaza mtu mwingine.

Nimesikia wimbo Mpya aliyouachia Msanii Roma Mkatoliki anayeishi ughaibuni akisema, "Roma tunakumisi rudi nyumbani". Sina hakika kama wapo wanaomkosa Roma.


Yote ni tisa. Kumi katika mistari ya Roma ambapo amevuka mstari mwekundu ni pale anaposema, "Mama (Samia) anaongoza yuko Ikulu lakini rimoti iko Msoga (Jakaya Kikwete).

Huku si tu Roma ametweza taasisi ya Rais lakini pia amemdharau na kumdhihaki Rais Samia Suluhu Hassan kwamba hawezi kuongoza hadi ashikiwe akili na Rais mstaafu Jakaya Kikwete jambo ambalo ni uzushi, uongo na upuuzi wa kisanii.

Roma haamini katika uwezo wa kiuongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan jambo ambalo limethibitishwa na jumuiya zote za Kimataifa kuwa anaweza na ameuthibiyishia Ulimwengu kuwa anaweza tena hata kuwapiku watangulizi wake.

Wimbo unatakiwa kupigwa ban kokote na popote, kuanzia mikusanyiko ya watu: baa, maafali, harusi, misinani, vyombo vya usafiri na hata watu binafsi nadhani TCRA wanaweza. Basata isilale huku Rais Samia Suluhu Hassan anadhalilishwa hadharani na msanii Roma.

Nani yuko nyuma ya Roma? Kiburi cha kumdhihaki Rais anapata wapi? Kwanini anachekewa? Kwani hafikiki? This is too much. Roma akamatwe na kuletwa hapa nchini tukutane Kisutu kwa Pilato. Ova.

Zaidi, soma: Nipeni maua yangu - Roma Mkatoliki
Nyie mlizoea utekaji na uuaji tu.
 
Hakuna nchi duniani inayoweza kuvumilia ukosoaji wa matusi kwa rais wake....haipo....

Tusijidanganye na iitwayo DEMOKRASIA ya ulaya kuwa kwa kiwango hichohicho cha kwao basi imeenea kwetu na tunaweza kuibeba 100p kama wao.....

Si lazima tafsiri ya DEMOKRASIA ya nchi za magharibi iweze kutekelezwa na kila nchi duniani....hapana huu ni uongo....

DEMOKRASIA ya magharibi inaendana na maisha yao ,TAMADUNI ,hulka ,mitazamo na vingi tu ambayo binadamu hatuwezi KUFANANA hata kidogo.....

Afrika ina TAMADUNI na maadili yake ambayo MATUSI haswa kwa waliotuzidi umri na walio viongozi wetu HAYARUHUSIWI/HAYAKUBALIKI hata chembe......

Huwezi kumdhalilisha rais namna vile alivyofanya.......

#SiempreJMT[emoji120]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Hajamdhalilisha mtu yeyote usitudanganye
 
CCM imetengeneza kizazi cha wapuuzi waimba sifa na mapambio, kiasi umeona katokea mwenye akili timamu hajaimba mapambio ya kumsifia rais chawa umeumia
 
Kuvuka mstari mwekundu🤔
Hizo sababu Sasa ulizotoa.
Jamani Freedom of expression ni lini itakuwa 100% Tanzania? Bora Roma huko alipo anajilipua tu
Maajabu ya Tanzania, Mtanzania anapinga Mtanzania mwenzake asipate haki au asiujue ukweli
 
Back
Top Bottom