Uchaguzi 2020 Msanii T.I.D aitaka CHADEMA imlipe kwa kutumia neno "Ni Yeyee" kwenye kampeni zao

Kama anayo hati miliki ya hiyo.. NIYEYE.. basi atalipwa mapema sana
Msanii Khalid Mohamed aka Top In Dar (TID) ameibuka na kutaka chama cha Demokrasia na Maendeleo kimlipe kwa kutumia neno "Ni Yeye" katika kampeni zao. Msanii TID anadai neno "niyeye" ni ubunifu wake

Lakini hata hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 5 hadi cha 7 cha Sheria ya Hakimiliki ya mwaka 1999, Copyrights and Neighbouring Act of 1999, "maneno" na "mawazo" ya wasanii si sehemu ya vitu vunavyotakiwa kulindwa chini ya Sheria hiyo.

Sheria hiyo imeweka wazi kuwa inalinda kwa lugha ya kisheria "expressions" and not "ideas".

Ijulikane wazi kuwa wazo linaweza kufanana na la msanii mwingine lakini namna ya kulieleza na kuliwasilisha wazo husika inaweza kuwa tofauti kabisa toka msanii mmoja hadi mwingine.

Kwa mfano wasanii wawili wanaweza kuwa na wazo la kuimba wimbo wa mapenzi wa mwanamke masikini kumpenda mwanaume tajiri lakini si rahisi kutumia beat na melody ya aina moja. Wanaweza pia wakajikuta wanatumia baadhi ya maneno sawa kwa mfano katika scenario hiyo neno kama " mapenzi" "nakupenda" etc yanaweza tumiwa na wote lakini kwa namna tofauti.

Hivyo kinacholindwa na sheria ni "expression" yaani ule ufundi na ubunifu wa msanii wa kulielezea jambo na siyo "maneno" anayotumia msanii wala "wazi" la msanii.

Isipokuwa tu maneno husika yawe yamesajiliwa chini ya sheria nyingine mfano kama trades mark au service mark ya bidhaa ya mhusika na anayetumia awe anatumia katika namna inayovunja haki au kuwachanganya wateja wa bidhaa hizo mbili. Jambo ambalo katika mazingira haya halipo.

Kwa vyovyote vile huwezi kusema kutumia kwa neno niyeye kwa CHADEMA achilia mbali tu kwamba halilindwi chini ya copyright laws bali tu hakuna madhara yoyote ya kiuchumi anayoyapata TID na vilevile CHADEMA hawalitumii kujiingizia pesa hivyo ni "fair use".

View attachment 1527556

TID kashindwa kupiga fedha kupitia bongo fleva sasa anazivizia za kupitia kwenye matango pori ya chakubanga
Ni Yeye ni kiswahili kinachotumika mdomoni mara kwamara.
Kumbe aje na mm ni mlipe.
 
Huyo ni wa kumpuuza tu maana hana tofauti na Stive Nyerere eti anaenda kumg'oa mh Msigwa iringa mjini na alicho kutana nacho kutoka kwa wajumbe hatokisahau.
Huyu naye njaa inamsumbua.
Hilo neno niyeye ni kiswahili tu cha kawaida ingekuwa hivyo hata aliyetunga kiswahili angekuwa anatudai pesa kwa kwa kutumia lugha yake ya kiswahili
 
Kuhusu ubunifu ni kweli yeye ndiye kalianzisha tatizo ni kama hana hatimiliki na hilo neno.

Kama kitu hakina hatimiliki ni unamaanisha kipo open kwa yeyote anayetaka kukitumia.
upuuzi.
 
Msanii Khalid Mohamed aka Top In Dar (TID) ameibuka na kutaka chama cha Demokrasia na Maendeleo kimlipe kwa kutumia neno "Ni Yeye" katika kampeni zao. Msanii TID anadai neno "niyeye" ni ubunifu wake

Lakini hata hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 5 hadi cha 7 cha Sheria ya Hakimiliki ya mwaka 1999, Copyrights and Neighbouring Act of 1999, "maneno" na "mawazo" ya wasanii si sehemu ya vitu vunavyotakiwa kulindwa chini ya Sheria hiyo.

Sheria hiyo imeweka wazi kuwa inalinda kwa lugha ya kisheria "expressions" and not "ideas".

Ijulikane wazi kuwa wazo linaweza kufanana na la msanii mwingine lakini namna ya kulieleza na kuliwasilisha wazo husika inaweza kuwa tofauti kabisa toka msanii mmoja hadi mwingine.

Kwa mfano wasanii wawili wanaweza kuwa na wazo la kuimba wimbo wa mapenzi wa mwanamke masikini kumpenda mwanaume tajiri lakini si rahisi kutumia beat na melody ya aina moja. Wanaweza pia wakajikuta wanatumia baadhi ya maneno sawa kwa mfano katika scenario hiyo neno kama " mapenzi" "nakupenda" etc yanaweza tumiwa na wote lakini kwa namna tofauti.

Hivyo kinacholindwa na sheria ni "expression" yaani ule ufundi na ubunifu wa msanii wa kulielezea jambo na siyo "maneno" anayotumia msanii wala "wazi" la msanii.

Isipokuwa tu maneno husika yawe yamesajiliwa chini ya sheria nyingine mfano kama trades mark au service mark ya bidhaa ya mhusika na anayetumia awe anatumia katika namna inayovunja haki au kuwachanganya wateja wa bidhaa hizo mbili. Jambo ambalo katika mazingira haya halipo.

Kwa vyovyote vile huwezi kusema kutumia kwa neno niyeye kwa CHADEMA achilia mbali tu kwamba halilindwi chini ya copyright laws bali tu hakuna madhara yoyote ya kiuchumi anayoyapata TID na vilevile CHADEMA hawalitumii kujiingizia pesa hivyo ni "fair use".

View attachment 1527556

Yesu Kristo NI YEYE yule Jana na Leo na hata milele. Awalipe kwanza wayahudi ndo madai yake yawe halali
 
TID ameshawishiwa na akina polepole kudai fidia bila kujua huyo msemo upo mtaani
 
Back
Top Bottom