Msanii Usher Raymond asikitishwa na mauaji ya Israel na Palestina, na kisha badae kufuta post hiyo huko Instagram

Msanii Usher Raymond asikitishwa na mauaji ya Israel na Palestina, na kisha badae kufuta post hiyo huko Instagram

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
Msanii kutokea nchini Marekani Usher Raymond katika mtandao wa Instagram ameonesha wasiwasi wake juu ya mambo yanayoendelea huko Israel na Palestina ikiwemo vifo vya watu zaidi ya 1000, utekaji wa wanaume, wanawake na watoto huku akisisitiza kuhusu kuzingatia uhai wa Bindamu, katika maelezo aliandika ujumbe unasomeka;

I pray for peace in the world in this dark hour. there are currently reports of over a 1000 innocent people murdered. As more and more images of men, women & children being released for the worlds reaction. i am more and more appalled. The sanctity of life should never be in a question... there should never be a debate. This is our humanity.

Ambao kwa kiswahili ukisomeka kama;
Ninaomba amani duniani katika saa hii ya giza. kwa sasa kuna ripoti za zaidi ya watu 1000 wasio na hatia kuuawa. Huku picha zaidi na zaidi za wanaume, wanawake na watoto zikitolewa kwa ajili ya miitikio ya walimwengu. nazidi kushangaa. Utakatifu wa maisha haupaswi kamwe kuwa katika swali ... kamwe kusiwe na mjadala. Huu ndio ubinadamu wetu.
Na katika picha akiambatanisha bendera ya Israel yenye neno "I Stand with Israel"

Screenshot_20231011-145943_1.jpg

Hata hivyo baadaye aliweza kuifuta post hiyo kwa sababu ambazo bado hazijafahamika. Ambapo ukipita kwenye Account yake uwezi kuikuta tena.
 
Nazani amefuta sababu ya kuomba amani huku umeshika au ficha panga

Una huzuni uku ukichagua upande wa kusimama, kama jaji mahakamani ana amua kesi akiwa kasimama upande mmoja wapo wa wanao subiri maamuzi

Nazani Usher amekubari kujikosoa na kuona post yake haikuwa na maana japo ina ujumbe mzuri
 
Yeah kaona mashabiki watakimbia 😂
 
Majibu atayapata mwakani kwenye tamasha lake.... wenzie walionyamaza kawaona wajinga.... yeye angeweka hata picha ya mshumaa tu na kuandika hayo aliyoyaandika na sio kuweka ushabiki mbele.
 
Back
Top Bottom