TANZIA Msanii wa maigizo maarufu Bi Sonia afariki dunia

TANZIA Msanii wa maigizo maarufu Bi Sonia afariki dunia

Inna lilahi wa inna ilahi rajiun. Rest easy bi.Sonia hakika uliutendea haki uhusika wako katika kila filamu. Very highly talented hakika tumepoteza jembe katika tasnia ya filamu.
 
Mungu awafariji wote walioguswa na msiba huu.
 
Pole nyingi kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki, pia na wale walioguswa na msiba huu wa Bi. Farida (Sonia). Mwendo ameumaliza nasi tuko njiani.
 
Pole kwa ndugu, jamaa na marafiki.
Bila shaka Steve Nyerere ata organize tukio vizuri.

''naenda kama Steve ukinikuta msibani, daftari likiniona linapata amani..."

NAENDA KAMA - by Nash Emcee a.k.a Mchochezi a.k.a Maalim a.k.a Zuzu.

-Kaveli-
 
Rest easy madam Sonia. Mwendo umeumaliza.

-Kaveli-
 
Halafu cha ajabu ITV huwa hawafanyi exclusive ya hawa wasanii ambao walifanya tupende kutazama channel zao.

Kwanini wasingekuwa wanaandaa special documentary ya hata nusu saa kuelezea maisha ya hawa wasanii na mchango wao katika sanaa ya tanzania na kuonyesha bidii yao ili kuwafanya vijana chipukizi kuwa na heshima na kujua mchango wao.

Kuna vijana wakimuona bi mwenda wanaona kaanza juzi kuigiza kumbe alianza na malijendi akina mzee pwagu na pwaguzi.

Mtu akimuona onyango wanajua ni mzee wa juzi kumbe weeee kaaanza miaka hiyo.
 
Akicheza nafasi ya mama, sauti yake vile anaongea Kwa upole na utulivu bila kubwatuka hovyo kama wasanii wengi "wanavyoigiza katika uigizaji wao". Tena enzi hizo kabla ya kampeni za kuwaasa waigizaji waache maigizo Bali wavae uhusika katika kazi zao, hakika alinikosha sana.
Hakika sote ni wa mwenyezimungu na kwake tutarejea.
 
Huyo mama alikuwa msanii halisi. Ni kipaji cha ukweli mnoo tumekipoteza. Mara zote nilipokuwa naangalia uigizaji wake nilikuwa nahisi haigizi bali alikuwa anafanya kitu halisi kwa 100%.
 
Jamani, amekufaje sasa!?
R.I.P bi sonia
 
Halafu cha ajabu ITV huwa hawafanyi exclusive ya hawa wasanii ambao walifanya tupende kutazama channel zao.

Kwanini wasingekuwa wanaandaa special documentary ya hata nusu saa kuelezea maisha ya hawa wasanii na mchango wao katika sanaa ya tanzania na kuonyesha bidii yao ili kuwafanya vijana chipukizi kuwa na heshima na kujua mchango wao.

Kuna vijana wakimuona bi mwenda wanaona kaanza juzi kuigiza kumbe alianza na malijendi akina mzee pwagu na pwaguzi.

Mtu akimuona onyango wanajua ni mzee wa juzi kumbe weeee kaaanza miaka hiyo.
Huo ubunifu waitoe wapi hao mkuu
 
Back
Top Bottom