Halafu cha ajabu ITV huwa hawafanyi exclusive ya hawa wasanii ambao walifanya tupende kutazama channel zao.
Kwanini wasingekuwa wanaandaa special documentary ya hata nusu saa kuelezea maisha ya hawa wasanii na mchango wao katika sanaa ya tanzania na kuonyesha bidii yao ili kuwafanya vijana chipukizi kuwa na heshima na kujua mchango wao.
Kuna vijana wakimuona bi mwenda wanaona kaanza juzi kuigiza kumbe alianza na malijendi akina mzee pwagu na pwaguzi.
Mtu akimuona onyango wanajua ni mzee wa juzi kumbe weeee kaaanza miaka hiyo.