KERO Msasa Gold Mine: Wachimbaji tumechoka unyonyaji. Kuna kiongozi anatamba akidai ana kinga ya Waziri wa Madini

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni Mwekezaji mdogo kwenye sekta ya uchimbaji (mchimbaji mdogo) kuna mazingira ya unyonyaji na uonevu unaoendelea kwenye Mgodi wa Msasa Gold Mine kwenye Mji wa Runzewe ambao umefumuka au kuibuka kipindi cha Uchaguzi Mkuu 2025, ukiwa unaendeshwa kama rush.

Awali, baada ya uvumbuzi wa wachimbaji wadogowadogo waliokuwa wanatafiti eneo hilo kukutana na mwamba wenye dhahabu ndani yake ikasababisha uanzishwaji wa ofisi (ofisi zinaratibiwa na mwenye leseni) ambapo kunakuwa na ofisi kuu ambayo iko chini kabisa ya wenye leseni ambao huwa wanachukua asilimia 20 ikifuatiza na ofisi ya shamba wanaochukua asilimia 10, pia kuna ofisi ya ulinzi na ofisi ya ukaguzi ambazo huwa na asilimia 5, asilimia nyingine ilio nje na hapo ni asilimia 7.1.

Pia, kuna asilimia 6 ya mrabaha wa Serikali, asilimia moja kodi ya Afisa Madini Mkazi na asilimia 0.1 kodi ya Serikali maalumu kwajili ya kuchangia mfuko wa UKIMWI, jumla ya asilimia huwa 40%.

Baada ya uzalishaji kuendelea na duara zikazidi kuongezeka pia mpaka kupelekea mgao kufanyika mara kadhaa kwa kutumia hizo asilimia ambazo wachimbaji huzitumia kwenye migodi inayoendeshwa kama rush.

Mwekezaji mdogomdogo hubakiwa na asilimia 60 ambapo pia yeye huwalipa watenda kazi asilimia 10 na kubakiwa na asilimia 50.

Sasa hivi imetokea sintofahamu baada ya hawa wasimamizi wa huu Mgodi kuunda mikataba upya ambayo ina asilimia tofauti ambazo ni za unyonyaji kwa wachimbaji wadogo (wazawa) wakilazimishwa kusainishwa mikataba kandamizi dhidi yao.

Wakishindwa kusaini, hao wamiliki kushirikiana na Kamati ya Usalama na Ulinzi Wilaya pamoja na Ofisi za Madini kwa ujumla wanafanya covering ya kuwatuhumu wachimbaji kuwa wanajihusisha na wizi wa mawe yanayosadikika kuwa yana dhahabu, hivyo kutumia silaha na nguvu zaidi kwa ajili ya kuwatawanya watu na kuzuia shughuli za uzalishaji kuendelea.

Asilimia zilizobadilishwa zina mtaka mwekezaji mzawa kwenye asilimia 50 anazobakiwa nazo azigawe tena kati kwa kati na wale wa ofisi kuu (wamiliki wa leseni) na kumlazimu mchimbaji huyu mdogo abakiwe na asilimia 25 ambapo ndio mwendeshaji wa duara (kwa maana ya kuwa yeye ndio mtoaji gharama zote na mzalishaji mkuu wa mgodi) Mwenye leseni anakuwa na jumla ya asilimia 75% na sio asilimia 20% ambazo ndio hutumiwa sehemu zote.

Pia, kumekuwa na hujuma ambazo hufanyiwa wawekezaji wadogo hapa mgodini kama kusimamishiwa kazi kila inapofika saa kumi jioni mpaka asubuhi ambazo hizo hujuma hufanywa na wasimamizi hao wa leseni kwa ajili ya kufanya wizi nyakati na usiku na kuiba stahiki za wawekezaji wazawa na kutorosha dhahabu hizo, hivyo kusababisha Serikali kuibiwa asilimia zake.

Kibuli hiki cha wamiliki wa leseni ni kutokana na;
a). Rushwa ambayo imekwisha tapakaa kwenye Kamati ya Usalama na Ulinzi Wilaya pamoja na Ofisi za Madini Wilaya na Mkoa ambao wanatoa kinga kwa wasimamizi wa mgodi kutokana na fedha walizo kula.

b) Mmiliki Mkuu wa Leseni (Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA), John Bina (ambaye ni Godfather wa waziri wa madini) ana kinga na Waziri wa Madini kiasi cha kupelekea Wasaidizi wake kutoa kauli kwa wachimbaji wadodowadogo kuwa wakashtaki wanapojua na yeye hawezi badilisha huo mkataba.

Anatamba kuwa yeyote ambaye hatosaini huo mkataba hatoruhusiwa kuendelea na shughuli zake za uchimbaji na atapewa kesi kama za kuanzisha vurugu, uhujumu uchumi n.k
 
Ama kweli umaskin ni laana kwenye nyakati hizi za uongozi huu
 
Ila haki, unyanyasaji, kutishana KUMEZIDI kwenye uongozi huu!
MPAKA LINI?!
 
Mwenye leseni eneo hilo anaitwa Cosmas Kisha ulizia ana undugu upi na katibu wa wizara ya madini bwana Sasamba.
Ukipata majibu jua kiburi kinatokea wapi.
 
mtoeni roho
 
Back
Top Bottom