MSD inalipa mshahara kwa mfanyakazi hewa (Laurean Bwanakunu)

kazi iendelee
 
Nimeuliza hiyo fixed contract yake ilikuwa ya muda gani? Nani anayejua kwamba imeisha au imevunjwa? Je kama haijaisha wala kuvunjwa sio halali yake kulipwa as per contract?
 
Hawa ndio wanapenda CCM iendelee na hawataku kusikia Katiba mpya majizi haya.
 
Check facts zako upya. Huyu hana kesi kuanzia June 2020 na siyo mfanyakazi wa MSD. Yuko mtaani na miahe zake lakini anakula mshahara wa MSD.
 
Magufuli hakuwa na akili , alijua anawakomoa watu kumbe anawapa shavu, unatengua wakurugenzi 200 unateua wengine 200 bila kujua wale uliotengua wanaendelea kula mishahara ya ukurugenzi, ameiongezea nchi madeni ya ajabu sana, na kwakua alikua kichaa wala alikua hashauriwi na mtu, mfano kulazimisha serikali kuhamia Dodoma ni uamuzi wa kiendawazimu kabisa , kapoteza fedha bila hata sababu ya msingi
 
Wamtafutie kazi ya kufanya sio kumpa mshahara bila kazi. Wahusika na huu ubadhilifu yafaa wachukuliwe hatua.
 
Taratibu za kutenguliwa ziko vipi? kwani kutenguliwa ni sawa na kufukuzwa kazi?
Tatizo wengi walikuwa wanaenda kwa mihemko, akitumbuliwa mtumishi wa umma wanafikiri mshahara unasimamishwa, ukitaka kuipaka matope legacy fanya uchunguzi ni wangapi wamelipwa kwa style hii🐒
 
Hiyo fixes Contract has no duration?kama wameona kuvunja mkataba itawagharimu hela nyingi,watakua sahihi kumlipa mshahara mpaka mwisho mwa mkataba
 
Stahiki (remuneration) za ile nafasi ndiyo hukoma mara baada ya kuondolewa madaraka uliyonayo.
Lkn mshahara ni haki yake, mpaka ajira itakapokoma.
Mkataba wake unasomeka vipi? Baada ya kuteuliwa mtu hupewa mkataba.Tusiongelee porojo weka mkataba
 
Ushahidi wa kuwa analipwa uko wapi?
 
Mkataba wake unasomeka vipi? Baada ya kuteuliwa mtu hupewa mkataba.Tusiongelee porojo weka mkataba

Hamna kitu kama mkataba wa uteuzi, ila kuna mkataba wa ajira. Uteuzi hufanywa kwa barua pekee.
 

ALIYEKUWA MKURUGENZI MSD AACHIWA HURU.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hii leo imewaachia huru aliyekuwa Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa,Laurean Bwanakunu na Mkurugenzi wa Logistik,Byekwaso Tabura baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kutoonyesha nia ya kutaka kuendelea na kesi hiyo
Bwanakunu na mwenzake walikuwa wakikabiliwa na mashitaka matano ikiwemo kusababishia MSD hasara ya Shilingi Bilioni 3.8 na kutakatisha fedha kiasi cha shilingi Bilioni 1.6.
Aidha kati ya Julai 2016 na Juni,30,2019 katika maeneo ya jiji la Dar es salaam Bwanakunu alidaiwa kuendesha genge la uhalifu pamoja na matumizi mabaya ya ofisi.

 
Hamna kitu kama mkataba wa uteuzi, ila kuna mkataba wa ajira. Uteuzi hufanywa kwa barua pekee.
Ok hiyo barua Ni mkataba pia hueleza terms zote.Kuanzia mshahara kipindi Cha kutumika na endapo hutataka kuendelea kwa sababu zozote iwe ugonjwa ,kifo etc au mteuzi atakupangia kazi ingine au kukutengua kabla ya muda inakuwaje.Nilishawahi ona barua ya mteuliwa mmojawapo aliteuliwa toka private sector kuwa mkuu wa idara moja ya serikali
 

Unaelewa maana ya mkataba wa ajira?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…