Msekwa: Yafaa spika kuwa mwanasheria, Spika Makinda asema si lazima

Msekwa: Yafaa spika kuwa mwanasheria, Spika Makinda asema si lazima

  • Spika atoke chama cha upinzani
  • Spika awe graduate wa sheria na uelewa mzuri wa sheria
 
Msekwa yuko Sawa.
Tatizo la kuchaguliwa Makinda lilitokana na mpango wa kifisadi wa kumzuia Sitta kuendelea na nafasi hiyo.
Pius anajua historia itakuja wasuta.
Anasema hivyo tokana na aibu inayosababishwa na undondocha unaoonyeshwa na makinda bungeni. Uozo huo wanauona.
 
Kazi ya wabunge ni kujadili miswaada inayoandaliwa kisheria na serikari. Miswada ile kuletwa bungeni ni kwa lengo la kupitiwa na wabunge ili waone kama ina maslahi kwa wananchi wote mbalimbali wanaowawakilisha.
Kwa msingi huo spika mwenye busara na utimamu wa akili anaweza kuongoza mijadala itakayofanywa na wabunge wote, akiongozwa na malengo ya kuweka sheria zitakazoboresha serikali na kuisaidia kuhudumia wananchi wake na kuleta maendeleo.
Bunge lisilo weza kuchanganua hoja za serikari na kuongeza njia bora zinazofaa kuondoa kero za wananchi na taasisi za serikari, si tu kwamba bunge hilo ni mzigo kwa serikari bali pia haliisaidii katika kufanikisha malengo yake.
 
Kama Mchangiaji moja alivyo sema Msekwa kaongea diplomatically, kwamba Mama ni vizuri akajishughulisha na kusoma sheria, ushauri wangu kwa huyu mama kama degree anaiona ni ndefu saana, basi afanye hata basic certificate ya sheria, hiyo ya kusomea uhasibu ni sawa ili mpa mwanga lakini kwake yeye inaonekana mwanga aliopata ni mdogo, jingine ni kupata mtu ampige shule ya hizo kanuni za bunge crash programme ya kama mwezi mpaka miezi mitatu, na aelewe ukiwa spika basi mambo ya chama chako unayaweka pembeni kidogo, sio kutumia nafasi yako kupinga hoja au kumwambia mtu akae chini nk nk, la sivyo hamna haja ya mijadala bungeni ikiwa matokeo yake ni utashi wa supika
 
Napingana na Mawazo ya Msekwa kuhusu kusomea sheria ili kuwa spika. Hauhitaji kuwa mwanasheria ili uwe spika. Unachohitaji ni uwezo wa kuelewa taratibu/kanuni ili uweze kuzitumia katika kuongoza mijadala bungeni. Bunge sio Mahakama hivyo kama anataka kujisifia na kumponda Makinda atumie gia nyingine. Hakuwa spika mzuri kwa mtazamo wangu na hiyo sheria aliyosomea haikumsaidia.
 
Msekwa alikuwepo wapi katika secretariate iliyompendekeza huyu mama? Maana wote walijua huyu siyo mwanasheria japo, atakuwa anafnaya kazi ya UANASHERIA
 
Makinda sio Spika ni kada wa Rostam, JK, Lowassa na mafisadi ccm. Kilichomweka ni dhambi na maovu yaliotendewa watanzania.
 
Wananchi tuamke majumbani na kuelekea bungeni kumtoa huyu fisadi mama. Chadema wakati umefika kufanya harakati za kumwondoa huyu fisadi na mkiukaji wa haki na demokrasia za wananchi. Bunge gani linalinda wezi na waharibifu wa resources za watanzania?
 
Huyu Msekwa ni mwanasiasa kimeremeta.Hung'ara usiku tu mchana ni kama wadudu wengine.Yeye Ni CCM mchana kama wenzake na usiku ni Chadema.
Anachofanya ni kuisaidia Chadema akidhani itashinda 2015.
Ikiwa alisomea sheria basi hakuelewa kitu darasani.Angalia alipokuwa spika alizuia uchunguzi wa mauwaji ya waislamu Mwembechai lakini akaruhusu uchunguzi wa mauwaji ya mbwa aliyeitwa Immigration.
 
Parliament of Tanzania. Pitieni hii profile link ya speaker Anne Makindi. Anaposema yeye ni professional accountant anaamanisha nn? Profile inasema alipomaliza Kilakala Girls Sec in 1970, alisoma Advanced Diploma ya ADMINISTRATION at the former Institute of Development and Management, currently Mzumbe University. Kwanini hayupo specific kama alisoma Advanced Diploma of Public Administration au hiyo ya finances, aitaje............ Na since hakuna sehemu inayoonyesha Mhe. Speaker since a-graduate IDM 1975 amesoma course yoyote, whether a short course or a long one. Labda wahasibu mnijuze, isn't finance a changing discipline? Just keen to know, nawasilisha....

Mhasibu kwa mujibu wa sheria ni yule aliyefaulu mitihani ya CPA na kusajiliwa na NBAA baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa. Ukimaliza CPA unakuwa kwenye kundi la wanaoitwa wahasibu wahitimu (Graduate Accountants). Ili usajiliwe rasmi inakubidi ufanye kazi za uhasibu ama ukaguzi kwa muda usiopungua miaka mitatu ili upate usajili unaoitwa ACPA (Associate Certified Public Accountant). Baadaye inabidi ufanye kazi kwa miaka mingine saba ili usajiliwe kwenye kundi la wahasibu mahiri la FCPA (Fellow Certified Public Accountant). Nimepitia orodha ya wahasibu ya NBAA mpaka sasa sijaona jina la Anne Makinda katika category yoyote ya uhasibu. Naendelea kutafiti kwani inawezekana alitumia jina lake la kusomea ambalo ni tofauti na hili la sasa.
 
Kazi ya wabunge ni kujadili miswaada inayoandaliwa kisheria na serikari. Miswada ile kuletwa bungeni ni kwa lengo la kupitiwa na wabunge ili waone kama ina maslahi kwa wananchi wote mbalimbali wanaowawakilisha.
Kwa msingi huo spika mwenye busara na utimamu wa akili anaweza kuongoza mijadala itakayofanywa na wabunge wote, akiongozwa na malengo ya kuweka sheria zitakazoboresha serikali na kuisaidia kuhudumia wananchi wake na kuleta maendeleo.
Bunge lisilo weza kuchanganua hoja za serikari na kuongeza njia bora zinazofaa kuondoa kero za wananchi na taasisi za serikari, si tu kwamba bunge hilo ni mzigo kwa serikari bali pia haliisaidii katika kufanikisha malengo yake.

Jamani tumsamehe bure huyu mama kwani vigezo muhimu vilivyotumiwa na CCM kumpa uspika ni jinsia yake ya kike na kuwepo kwake bungeni kwa muda mrefu. Haya mambo yenu mengine ya usomi wa sheria hayakuwa ya msingi sana wakati wakifanya maamuzi ya kumteua awe spika.
 
Nilipoona hii thread kitu cha kwanza kujiuliza ni hiki cha uwepo wa Msekwa wakati wa kumpendekeza huyu mama........................ Thanks Samora kwa kuwahi.........

Inawezekana "amejivua gamba" wandug, msameheni bure!
 
Sitashangaa wakimtimua kazi kwa kuwahofia wabunge machachari wa chadema wanaojua sheria na kumdhalilisha speaker na ccm yake.
 
Sitashangaa wakimtimua kazi kwa kuwahofia wabunge machachari wa chadema wanaojua sheria na kumdhalilisha speaker na ccm yake.

Nadhani ndio wanakoelekea si unawajua tena wanaanzisha zengwe kupitia maneno lakini ujue tayari wameangalia wanaona vijana wamemzidi kete watamfukuza hawana agenda ya kudumu CCM wameshamtumia watamtupa kama tambala bovu
 
Msekwa alikuwepo wapi katika secretariate iliyompendekeza huyu mama? Maana wote walijua huyu siyo mwanasheria japo, atakuwa anafnaya kazi ya UANASHERIA
Marando aliwaambia nafasi ya Uspika inafaa ikaliwe na mwanasheria lakini wakampigia kura kwa kishindo wamuache aendeleze libeneke wanaona aibu kungali mapema
 
Msekwa yuko Sawa.
Tatizo la kuchaguliwa Makinda lilitokana na mpango wa kifisadi wa kumzuia Sitta kuendelea na nafasi hiyo.
Pius anajua historia itakuja wasuta.
Anasema hivyo tokana na aibu inayosababishwa na undondocha unaoonyeshwa na makinda bungeni. Uozo huo wanauona.

uko sawa kabisa mjomba
 
Back
Top Bottom