Msemaji Mkuu wa serikali atoa uamuzi wa Baraza la Mawaziri kuhusu Ajali ya ndege Bukoba

Chief safari ilikuwa Dsm to Mz kupitia Bukoba
 
Yaani Msemaji amekuwa mkubwa kuliko Mkuu wa Majeshi Tz. Tz ina vituko balaaa
 
Msigwa sijui namuonaje hana radha tena ya usemaji na hana test ya usemaji wenye viwango. wamtafutie kitengo kingine basi.
Mimi pia ninamuona Msigwa, kwa namna anavyoisemea serikali ni mtu asiye na exposure yo yote ile ya masuala iwe ya kijamii, uongozi, diplomasia, mahusiano iwe public au International relation au cho chote kile. Inaonekana alibebwa tu kwa kujuana na magu

Nilitegemea kuwa msemaji wa serikali anaweza kuwa mtu mahiri katika nyanja nyingi na mwenye haiba ya kidiplomasia, lakini huyu jamaa yuko tofauti kabisa, amejaa mipasho kama mwandishi wa udaku.

Huyu si wa kupewa kitengo cho chote, ni bora wampeleke akanolewe katika iternational relations. Hiyo kozi itamsaidia sana.
 
Mbona mabasi yakiuwa baraza la mawaziri halikai? Au wapanda ndege ni bora kuliko wapanda mabasi?

Ni kwa sababu wapandaji ndege ni wao na familia zao hivyo ajali imewafikia, mabasi wanaopanda siyo watu muhimu hapa Tanzania.

Kwa kifupi ni ubinafsi na they don’t care about us!
 
It's either siasa zimefeli Taifa hili na sasa tunavuna matokeo yake.
 
Tulijua tuu ni bla blaa. Ccm haija wahi kuwa na nia njema na raia wake. Story ya Majaliwa imekuwa ya zamani sasa wana tengeneza tukio jingine. Kusubiri ripoti ya tume. Iwekwe kapuni. Majaliwa Pm ana ripoti ngapi kaweka kwapani?
 
Mbona mabasi yakiuwa baraza la mawaziri halikai? Au wapanda ndege ni bora kuliko wapanda mabasi?
Mi nimekereka mno, watu wanakufa kila uchao, hakuna anaekaa kutaka kujua chanzo cha hivyo vifo ila ndege mara moja kwa miongo kadhaa wapuuzi wanakaa vikao kwa kodi zetu na mashangingi ya mamia ya mamilioni kujadili.

Idiot
 
Njia za usafiri ziko kadhaa ambazo ni barabara, anga, maji, reli na mawasiliano mtandao.

Laiti ingekuwa ajali ya ATCL kuna balaa lingetokea kwenye utawala ni lawama zote angetupiwa JPM. Hata sasa hao hao kwa kupitia mlango wa nyuma wanasingizia alipoka haki ya uwanja wa ndege kujengwa Bukoba akaelekeza ujengwe Chato kitendo ambacho kimesababisha ajali ya ndege!!!!

Mashuhuda waliokuwemo kwenye ndege na waliokuwa ardhini wanakiri siku hiyo kulikuwa na mvua, mawingu mazito kiasi ambacho huwezi kuona uwanja wenyewe sijui huo uwanja unaodaiwa laiti ungekuwa umejengwa huko Bukoba ungeepushaje hiyo ajali?

Huyo mvuvi Majaliwa aliye-trend sana na kupewa shavu la kwenda kusomea uokoaji ni kada wa CCM ambaye katibu wa chama chao amekiri na kumtambua.

Swali linakuja, je baada ya Majaliwa kufunga kamba kwenye mtumbwi na ndege ili kuivuta lakini isivyo bahati kamba ikakatika na kumpiga kwenye paji la uso kisha kuzimia akiwa majini, ni nani alimwokoa na kumpeleka nchi kavu kisha hospitali?

Kwanini waliomwokoa Majaliwa hawajafikiriwa kwenda kuchukua mafunzo ya uokoaji kama sio ubaguzi wa kisiasa?

Je, huyo mvuvi aitwaye Majaliwa sio kwamba ni moja wapo wa vijana wanaochomekwa na idara ya usalama kwa malengo maalum katika maeneo tofauti ikiwemo kwenye shughuli za uvuvi ili asitambulike katika jamii aliyochangamana nayo kufanikisha kazi ya ukusanyaji wa taarifa nyeti?
 
Huyu si walimuondoa Ikulu, sasa baraza linasemewa na msemaji wa Ikulu au wa serikali kwa ujumla, hiki kikao ni cha Ikulu nilidhani msemaji wa Ikulu ndio angejitokeza
 
pamoja na kupata promosheni lakini kuwa mkuu wa idara ya habari na mawasiliano ikulu ni kitu kikubwa kuliko kukaa pale kwenye zile ofisi karibu mnara wa askari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…