Msemaji Mkuu wa Serikali: Serikali inafuatilia kwa ukaribu mijadala ya JamiiForums, ile ya kufaa itachukuliwa na kufanyiwa kazi

Msemaji Mkuu wa Serikali: Serikali inafuatilia kwa ukaribu mijadala ya JamiiForums, ile ya kufaa itachukuliwa na kufanyiwa kazi

Tunawakaribisha,
Maana tunaamini serikali ipo kila mahali..
Safii sana msemaji mkuu
 
Kwangu wasijaribu kabisa!
Wakijichanganya wakasoma za kwangu na mtoto wa mama mkwe watakufa kabisa sio kuzimia tu!
Sasa kwa hivi ulivyosema hapa si utafanya wakija waanze na wewe ili waone kama watazimia kweli kwa hayo mambo yenu na huyo mtoto wa mama mkwe wako? Lol

Ova
 
Sasa kwa hivi ulivyosema hapa si utafanya wakija waanze na wewe ili waone kama watazimia kweli kwa hayo mambo yenu na huyo mtoto wa mama mkwe wako? Lol

Ova
Mtoto wa mama mkwe anapomuongelea mtoto wa mama mkwe!
 
Kama kweli sarikali inafuatilia huu mtandao, niwaone Tanroads au wizara ya ujenzi wakijibu hii reply. "Barabara ya mbezi high school kwenda mpigi magoe kupitia machimbo inakera sana. Kwa sasa imekuwa mahandaki tupu! Karne ya 21 Tanroads ina barabara za vumbi Dar es Salaam, mkoa unaoingiza asilimia zaidi ya 70 kwenye mapato ya serikali ya kila mwaka. Daaah inasikitisha sana. Au hizi barabara zinaachwa kama michongo kwa ajili ya kuchongwa chongwa?"
 
Back
Top Bottom