Msemaji Mkuu wa Serikali: Vyombo vya habari vya ndani vitawajibika kama vyombo vya habari vya nje walivyojiunga navyo vitakiuka sheria ya habari

Msemaji Mkuu wa Serikali: Vyombo vya habari vya ndani vitawajibika kama vyombo vya habari vya nje walivyojiunga navyo vitakiuka sheria ya habari

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Wakuu, Hassan Abbas (Daktari) ambaye ni msemaji mkuu wa serikali ameweka rasmi kofuli la uhuru wa habari Tanzania.

Akitoa ufafanuzi leo anasema "Leseni mpya ya vyombo vya habari vya ndani ambavyo vinataka kujiunga na vyombo vya habari vya nje inavielekeza kuwajibika kama vyombo hivyo vya nje vitatoa habari inayokiuka sheria mpya ya habari.

Kama hamjui sheria mpya ya habari ni mbaya sana. Kwa mfano ingekuwa kile kipindi cha Corona basi kwa sheria hii Star tv wangefunga kituo maana daily wangelimwa faini milioni 15.

Kwa wasiojua ni kuwa sheria hii inatamka wazi kuwa habari yoyote ile hata kama ni ya kweli basi itakuwa halali tu pale ambapo imethibitishwa na Serikali na mamlaka zake zilizowekwa kisheria. Mbaya sana hii!

Nakupa mfano tetemeko la jana hata kama watu walilisikia basi kama halijatangazwa na chombo husika kilichowekwa na serikali bado siyo tetemeko na ikilitangaza unachukuliwa hatua.

Huu utawala huu ni utawala wa aina yake! Yani kwa mfano Lissu alipopigwa risasi basi ni mpaka mamlaka husika yaani jeshi mapolisi liseme kuwa Lissu kapigwa risasi ndipo itangazwe! Hata kama umeshuhudia akipgwa risasi basi hesabu kuwa hujashuhudia.
 
Ndio maana siku zote huwa nasema humu hawa watu wamenyimwa maarifa ili utawala wao ufike mwisho.

Mambo haya kisiasa, kimataifa,kijamii,n.k , ni blunders kubwa sana zitazowagharimu vibaya mno CCM .

Wapinzani hii iwe ni moja ya agenda yenu kuu katika kampeni za mwaka huu.

Hata hivyo, nashukuru maamuzi haya kwani yatasaidia "slow leaners" katika siasa kuelewa maneno ya wapinzani kama Tundu Lissu kuwa hakuna alie salama.
 
Hii sheria mpya ya vyombo vya habari ni ya "KIWENDAWAZIMU". Ila acha kina MillardAyo akili ziwakae sawa, acha vyombo vyote vya habari waendelee kuunga juhudi tu, juhudi zenyewe ndio hizi sasa. Wasilalamike
 
kifo cha ccm kimewadia na kinafia mikononi mwa Maraika mkuu,jiwe hanasifa za kuwa kiongozi ,waliompa wamejitenga naye wameachia jahazi ,na jahazi limeshaanza kuzama
 
Back
Top Bottom