Hawa vigogo wa vyombo vya serikali ya Ayatollah Wajisalimishe, hakuna namna watapona mkono wa operesheni EPIC FURY wala operesheni Roaring Lion
19 March 2026
Taarifa ya Waziri Mkuu Netanyahu kwa Vyombo vya Habari vya Kigeni
View: https://m.youtube.com/watch?v=kqGs6HEwd-c
SCRIPT
"Kwanza kabisa, nataka tu kusema kwamba niko hai, na nyinyi nyote ni mashahidi."
Sasa kwa kuwa nimeondoa habari hii ya uongo feki, nataka kuwapa taarifa mpya kuhusu Operesheni ya Kunguruma Simba Roaring Lion . Chini ya uongozi wa maono wa Rais Trump, Amerika na Israeli wanashirikiana nchini Iran kwa kuongoza kampeni ya nguvu isiyo na kifani dhidi ya utawala wa kiwendawazimu wa Ayatollah.
Operesheni ya Ngurumo ya Simba imeundwa kuondoa vitisho vinavyotokana na utawala wa Ayatollah, utawala ambao umepigana vita dhidi ya Amerika na Israeli na watu wa Iran kwa miaka 47. Wakitamba na, Kibwagizo cha kaulimbiu 'Kifo kwa Amerika, Kifo kwa Israeli, na pia inawapa watu wake kifo.
Malengo yetu ni matatu. Moja, kuondoa tishio la nyuklia. Pili, kuondoa tishio la makombora ya masafa marefu na kuondoa vitisho hivi vyote viwili kabla havijafichwa kwa kuzikwa chini ya ardhi ndani ya mahandaki marefu na kuwa kinga dhidi ya mashambulizi ya angani. Na tatu, hii ina maana ya kuunda mazingira kwa watu wa Irani kufahamu uhuru wao, kuchukua hatima yao mikononi mwao wenyewe.
Leo, utawala wa Ayatollah haushambulii Amerika tu, haushambulii Israeli tu, haushambulii watu wa Iran tu, bali pia unashambulia Mashariki ya Kati nzima na kwingineko. Wameshambulia raia na Wamarekani na mali za Marekani nchini Iraq, Kuwait, Saudi Arabia, Bahrain, Qatar, UAE, Oman, na hata wamethubutu kushambulia nchi ya Cyprus iliyo barani Ulaya kwa kutumia vikaragosi vyao waliopo Lebanon.
Tumeonya kwa miongo kadhaa kwamba mpango wao wa makombora ya masafa marefu utatumika kushambulia maeneo mbalimbali, na ikiwa hawatazuiwa, huo ni mwanzo tu.
Vibwagizo vyao vya 'Kifo kwa Marekani na Kifo kwa Israel' vinavyoimbwa nchini Iran na kujaribu kuitisha dunia kwa kufunga njia muhimu ya kimataifa ya baharini, Mlango wa Hormuz usifanye kazi. Israeli inasaidia kwa njia yake, kwa akili na njia zingine, juhudi za Marekani za kufungua mlango wa bahari wa Hormuz.
Lakini nataka kukuuliza ufikirie jinsi utawala wa Ayatollah ungeweza kuitisha dunia nzima ikiwa ungekuwa na makombora ya masafa marefu yenye vichwa vya silaha kali ya nyuklia. Hebu fikiria wangefanya nini.
Angalia wanachofanya sasa na fikiria wangefanya nini kama wangekuwa na makombora ya balestiki, makombora ya balestiki ya masafa marefu ya kimataifa na vichwa vya nyuklia. Hebu fikiria tu jinsi ingeweza kuwa tishio kubwa.
Kwa hivyo leo Israeli na Marekani kupitia operesheni hii dhidi ya utawala wa Ayatollah wanailinda si tu Amerika, Israeli, Mashariki ya Kati nzima, lakini nathubutu kusema dunia nzima. Licha ya habari bandia ambazo kwa bahati mbaya zimesambazwa tangu kuanza kwa vita siku 20 zilizopita, tunashinda, na Iran inaangamizwa.
Silaha za makombora na ndege zisizo na rubani za Iran zinaharibiwa kwa wingi sana na zitaharibiwa. Mamia ya silaha vifyatuaji vyao vimeharibiwa, akiba yao ya makombora inapigwa vikali, na vivyo hivyo viwanda vinavyoyazalisha silaha na zana hizo. Hilo ni muhimu.
Katika operesheni Rising Lion 2025 Simba ananyanyuka, tuliharibu makombora na tukaharibu miundombinu mingi ya nyuklia. Lakini tunachoharibu sasa ni viwanda vinavyozalisha vipengele vya kutengeneza makombora haya na kutengeneza silaha za nyuklia ambazo wanajaribu kutengeneza. Tunaangamiza kambi yao ya viwanda kwa njia ambayo hatukuwahi kufanya hapo awali.
Ulinzi wa anga wa Iran umefanywa kuwa hauna maana kwani umetepeta. Jeshi lao la wanamaji liko chini ya kilindi kirefu cha kina cha bahari baada ya kuangamizwa kwa mashambulio yetu. Leo tunapiga sehemu nyingine ya jeshi lao la wanamaji katika Bahari ya Caspian kaskazini mwa Iran. Jeshi lao la anga karibu liangamizwe.
Muundo wa kijeshi na vyombo vyote vya kutoa amri na udhibiti wa jeshi na vyombo vya Iran uko katika makanganyiko mkubwa kwa makamanda wao wakuu na maafisa waandamizi kuuawa. Na naweza kukuambia kwamba bado kuna kazi zaidi ya kufanya, na tutafanya hivyo.
Na ninataka kupinga minongono ya matamshi ya uzumii wa habari nyingine ya uongo feki, na hiyo ni kwamba Israeli kwa namna fulani iliiingiza Marekani katika mgogoro na Iran. Je, kuna mtu yeyote anayefikiri kweli kwamba mtu anaweza kumwambia Rais Trump la kufanya? Haya. Rais Trump hufanya maamuzi yake kila wakati kuhusu kile anachofikiri ni kizuri kwa Amerika, na naomba niongeze, nadhani anafanya kile ambacho pia ni kizuri kwa vizazi vijavyo. Katika hali hii, maslahi hayo yako wazi kabisa, na hivyo ndivyo ilivyo wazi kwa mafanikio yetu. Pamoja kwa ushirikiano wa karibu na Rais Trump, ushirikiano wa karibu kati ya Amerika na Israeli, wanajeshi wetu, huduma zetu za ujasusi, tunafikia malengo kwa kasi ya umeme.
Lakini nataka kusema neno lingine. Imesemwa kwamba kwa miaka 40 nimekuwa nikisema kwamba Iran ni hatari kwa Israeli na hatari kwa ulimwengu. Hiyo ni kweli. Unajua ni nani mwingine aliyesema hivyo? Rais Trump, miaka 47 iliyopita, wakati majambazi wa Iran walipoteka majengo ya ubalozi wa Marekani, alisema jinsi utawala huu ulivyo hatari. Katika muhula wake wa kwanza ofisini, hakuhitaji kushawishiwa. Alisema makubaliano ya maridhiano kuhusu nyuklia na Iran yalikuwa makubaliano mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa, na akajiondoa. Kabla tu ya muhula wake wa pili, kabla ya kuchaguliwa tena, nilienda kumwona Florida huko Mar-a-Lago. Jambo la kwanza aliloniambia lilikuwa, Bibi (a.k.a Netanyahu), tunapaswa kuhakikisha kwamba Iran haina silaha za nyuklia. Aliniambia hivyo. Sikumwambia. Hakuhitaji kushawishiwa kuhusu jambo hilo.
Sasa kwa nini alisema hivyo? Kwa sababu kwa zaidi ya miongo minne, utawala huu, kama nilivyosema mwanzoni mwa hotuba zangu, wimbo wa jaramba la utawala wa Ayatollah wakijipiga vifua , wa 'Kifo kwa Israeli, Kifo kwa Amerika.
Lakini Iran wanasema Israeli ni Shetani mdogo tu anayesimama njiani mwao. Shetani mkuu ni Marekani. Na hawa washabiki wa kiitikadi kali, hawa wapumbavu, wanaona sababu yao ya kuwepo, ni kufuta ustaarabu wa Magharibi na Amerika inayoiongoza. Wamesitisha maisha, wamewajeruhi na kuwajeruhi maelfu ya Wamarekani nchini Iraq na Afghanistan. Waliwaua wanajeshi wa Marekani huko Beirut. Walipiga mabomu balozi zenu.
Walijaribu kumuua rais wa Marekani, Donald Trump, si mara moja bali mara mbili. Sasa wanatutishia kwa mafuta. Hebu fikiria wangefanya nini, wanachoweza kufanya, kama hawa wapumbavu wendawazimu wangekuwa na silaha za nyuklia na njia za kuzivyatua masafa marefu hadi kufikia kila mji wa Marekani na kila mji wa Ulaya na kila mahali duniani kote. Hii ni hatari kwa ulimwengu mzima. Hakika ni hatari kwa Israeli. Hakika ni hatari kwa Amerika.
Hatupepesi macho kuhusu hilo, mimi na Rais Trump, Israeli na Amerika. Lakini nadhani ikiwa watu ni waaminifu, ikiwa viongozi ni waaminifu, wangeelewa kwamba hatupigani vita vyetu tu, bali pia tunapigana vita vyao.
Ninazungumza na viongozi kadhaa wa dunia, makumi kadhaa. Wote waunga mkono na najua msimamo huo wa Trump. Na tukiwa faragha, wote wanasema hivyo. Wanasema hivyo faraghani, lakini mimi sijifichi nasema hivyo hadharani. Dunia ina deni kubwa la deni kubwa, deni kubwa, kwa Rais Trump kwa kuongoza juhudi hizi za kulinda mustakabali wetu
Source :
https://www.gov.il/en/pages/spoke-statment190326