Msemaji wa klabu ya yanga anatakiwa kuwa muungwana

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
1,289
Reaction score
2,199
Msemaji wa Klabu ya Yanga kila mara amekuwa akitoa maneno yasiyo na staha. Mfano hai ni pale alipokuwa mjini Tabara alitamka wazi kuwa Mkuu wa Mkoa hataalikwa kuja kula nyama siku ya Iddi. Kwa maneno mengine Mkuu wa Mkoa ndiye Mwakilishi wa Rais katika Mkoa ule ni kama maneno hayo alimuelekezea Mhe. RaIs. Nashauri viongozi wa Yanga mkae naye na apewe onyo kwa maneno anayoyatoa ambayo hayana maana. Heshima ni kitu cha bure ni vema akaonyesha heshima mbele ya wakubwa wake.
 
Sasa kama Mkuu wa Mkoa mwenyewe ameamua kujigeuza kuwa kituko na pia mchekeshaji, shida iko wapi kwa huyo Ali Kamwe kumpa haki yake anayostahili? Huyo Mkuu wa Mkoa hawezi kuheshimiwa, kama yeye mwenyewe tu hajiheshimu.

Mambo ya kufanywa na Christina Mwagala, ameona ayafanye yeye! Hivyo anastahili kabisa kudharauliwa, na pia kukejeliwa ili siku nyingine ajifunze kuweka mipaka kati ya ushabiki na hicho cheo chake.
 
Aliwahi kusema Juma Mgunda akili zake kama maandazi
Hana adabu dogo
Tatizo watoto waliolelewa na single maza
 
Msemaji wa Klabu ya Yanga kila mara amekuwa akitoa maneno yasiyo na staha. Mfano hai ni pale alipokuwa mjini Tabara alitamka wazi kuwa Mkuu wa Mkoa hataalikwa kuja kula nyama siku ya Iddi. Kwa maneno mengine Mkuu wa Mkoa ndiye Mwakilishi wa Rais katika Mkoa ule ni kama maneno hayo alimuelekezea Mhe. RaIs. Nashauri viongozi wa Yanga mkae naye na apewe onyo kwa maneno anayoyatoa ambayo hayana maana. Heshima ni kitu cha bure ni vema akaonyesha heshima mbele ya wakubwa wake.
Akaonyesha ❌
Akaonesha ✅

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Katika hili Ali Kamwe yupo sahihi, mkuu wa Mkoa kajisahau nafasi yake akageuka kama mtu mlevi vile. Eti anashangaa kwanini Ali Kamwe kapokelewa na watu wengi, mara anaituhumu Yanga kwa kuwapa rushwa wachezaji wa Tabora. Sasa mkuu wa mkoa ni serikali na kuna TAKUKURU ambao anaweza kuwaamrisha wafanyie kazi hilo jambo iweje analia lia kwenye vyombo vya habari na mitandaoni kama hilo swala lina ukweli?
 
Sasa kama Mkuu wa Mkoa mwenyewe ameamua kujigeuza kuwa kituko na pia mchekeshaji, shida iko wapi kwa huyo Ali Kamwe kumpa haki yake anayostahili? Huyo Mkuu wa Mkoa hawezi kuheshimiwa, kama yeye mwenyewe tu hajiheshimu.

Mambo ya kufanywa na Christina Mwagala, ameona ayafanye yeye! Hivyo anastahili kabisa kudharauliwa, na pia kukejeliwa ili siku nyingine ajifunze kuweka mipaka kati ya ushabiki na hicho cheo chake.
Utakuwa ndo wewe hapo. Jirekebishe
 
Sasa kama Mkuu wa Mkoa mwenyewe ameamua kujigeuza kuwa kituko na pia mchekeshaji
Hata Samia ni kituko na mchekeshaji je mmewahi kutomheshimu?

Wasira naye hivyo hivyo...

Sema tu RC Chacha sio mtu wa visasi japo anao uwezo wa kumlaza sero huyo dogo wenu mbulula.

Msaidieni kijana awe na adabu kwa wenye mamlaka kabla hajakutana na mwenye mamlaka kichaa wa kumlaza lockup
 
Ishu ni kuwa hawa wakuu wa mikoa kujiingiza kizabinazabina kishabiki na kuzikumbatia timu zao kama pamba na tabora united wakuu wa mikoa hiyo walikutana na zahma za wasemaji wa simba na yanga, waacheni wale za uso kishabiki. Mbona yule wa singida iliko black stars, coastal union, kagera sugar, mashujaa, namungo wakuu wa mikoa hiyo hawajajitokeza kindezi kushabikia timu za maeneo yao? Au kwa sababu sio timu za taasisi za umma? Kuna dodoma jiji, kmc hatujaona wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi wa halmashauri wakijitokeza na kula za uso toka kwa wasemaji wa simba na yanga. Acheni hao wakuu wa mikoa wale za uso kishabiki
 
Hata Samia ni kituko na mchekeshaji je mmewahi kutomheshimu?

Wasira naye hivyo hivyo...

Sema tu RC Chacha sio mtu wa visasi japo anao uwezo wa kumlaza sero huyo dogo wenu mbulula.

Msaidieni kijana awe na adabu kwa wenye mamlaka kabla hajakutana na mwenye mamlaka kichaa wa kumlaza lockup
Mumshauri Mkuu wenu wa Mkoa asijisahau! Hata kama yeye anajitambulisha/mnamtambua kama mlezi wa timu, bado haimpi haki ya kujiingiza kwenye siasa za mpira! Halafu ategemee kuachwa tu hivi hivi, eti kwa sababu ni Mkuu wa Mkoa.

Nitaendelea kurudia! Alichokifanya Ally Kamwe ni kitu sahihi kabisa. Na huyo Mkuu wa Mkoa hana hiyo jeuri ya kumuweka Ally Kamwe ndani! Kwa sababu amejibiwa kama Chacha, na pia kulingana na matamshi yake aliyo yatoa hapo kabla dhidi ya timu ya Yanga! Na hakujibiwa kwa sababu ya cheo chake.
 
Sasa mualiko wa nyama ya Eid ni jambo la kuandikia uzi kweli.
 
Msemaji wa Klabu ya Yanga kila mara amekuwa akitoa maneno yasiyo na staha. Mfano hai ni pale alipokuwa mjini Tabara alitamka wazi kuwa Mkuu wa Mkoa hataalikwa kuja kula nyama siku ya Iddi. Kwa maneno mengine Mkuu wa Mkoa ndiye Mwakilishi wa Rais katika Mkoa ule ni kama maneno hayo alimuelekezea Mhe. RaIs. Nashauri viongozi wa Yanga mkae naye na apewe onyo kwa maneno anayoyatoa ambayo hayana maana. Heshima ni kitu cha bure ni vema akaonyesha heshima mbele ya wakubwa wake.
Tumewndekeza sana hao bijana

Wote wawili
 
Swali fikirishi kwanini walizuia amsha amsha, (vibe) la mzuka wa mashabiki wa yanga? Sinto fahamu itakuwa ilianzia hapo

Public figures have to keep their words

Viongozi wa kitaifa inatakiwa wachunge kauli zao , Tanzania viongozi wa kitaifa hawana uwezo wa kutunza kauli zao
 
Mkuu wa mkoa amekuwa msemaji wa timu!, Aliyoysema alipaswa ayaseme mwagala na sio level ya ukuu wa mkoa!!. Simba na yanga ukiziendea vibaya inatia mchanga kitumbua chako.
 
Back
Top Bottom