Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Toka lini mtu akamshauri adui yake ili afanikiwe? Hii mpya sasa. Lkn kwani alichosema lisu ni uongo? Kama ni kweli shida iko wapi? Z. Kawawa amekiri kwa niaba ya serikali, sasa wewe mini tatizo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo ni gazeti limewanukuu
gazeti gani mkuu, tz daima au mwanahalisi?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mme
Hao ni wasomi wachumia tumbo, hv hata msukuma ni msomi? Nimemsikia akimponda lissu
Mmekaribisha mafisadi wanawafundisha namna ya kufisadi Nchi kwa elimu mlopewa kwa jasho la watz. Wenzenu watavuta dola nyie mnasubiri Diamond nuts na sayona juice. TL na genge lake likiongozwa na Fisadi Mkuu wana stahili kuhojiwa kwa uhujumu uchumi wa Nchi. Na nyie mtakwenda kusaidia
 
Nimesoma sakata la kuzuiwa kwa ndege aina ya mbombardier nchini Canada kutokana na hukumu ya Mahakama iiiyowekwa. Binafsi tusimlaumu Mhe. Rais kwa sakata hili. Mhe. Rais hahusiki hata kidogo LAKINI yule Waziri aliyesababisha tatizo hili AKAMATWE mara moja ili awajibike. Pia nawashauri CCM watu kama hawa msiwe mnawapitisha kugombea Ubunge wakati mnafahamu mienendo yao na jinsi walivyolitia Taifa hasara kubwa. Mpaka sasa bado wanapeta pale mjengoni. Hii ni fedheha sana kwa nchi.
 
Upinzani wa awamu hii umekosa agenda, agenda yao ni kupinga maendeleo
 
Ni wasomi kuwa wanavyeti bàada ya kumaliza vyuo au ni wasomi kwa kuwa wanaujuzi,maarifa na uwezo wa kufikiri na kutazàma mambo kwa upana wake? Ninachojua Mimi Lissu amekuwa àkisema nini kifanyike kila nchi inapokuwa nà mgogoro has a unàhusu sherià,ilà watu wànaofañya siasa nyepesi huwa hawataki kutumia ushauri wake kwa kuogopa kumpa umaarufu kwa kuwa wao madaraka yao na kuwepo kwao madarakani ni muhimu zaidi kuliko nchi yetu.Hao wasomi,watakuwa wasomi cheti tu
 
umekosa exposure na kuwa brain washed na siasa nyepesi, si kosa lako,pole
 
Waziri yupi aliyesababisha Mkuu
Mbona unakurupuka tu kuanzisha Uzi
Aliyesababisha hilo sakata ni waziri wa ujenzi wakati huo John pombe Magufuri sasa unataka tumfanyaje Rais wetu kwa mfano
 
Kama tunakumbuka hapo awali na mara kadhaa Mh Rais Magufuli amesisitiza tumuombee kwani vita alivyoingia ni vita vya kiuchumi vinavyogusa maslahi ya watu wazito na wenye ukwasi wa kutosha.

Toka vita hii au niseme mchakato huu uanze pamekuwa na jitihada nyingi za kuhakikisha Tanzania haifanikiwi,Kumekuwepo na jitihada kubwa za kuingilia Tume wakati ule wa uchunguzi.

Tulisikia watu akiwemo Tundu lisu kufanya jitihada kubwa za kutaka kupata taarifa za mwenendo wa Tume za Makanikia.Tulisikia wajumbe wa Tume wakitaka kuhongwa ili kuvuruga ushahidi na uchunguzi.

Hii ilimaanisha kuwa kulikuwepo na bado kuna mipango miovu ya aina yote ya kutaka kuihujumu Tanzania mara baada ya kutaka kudai haki yetu na fedha zetu zilizoporwa kwa miaka kadhaa huku wananchi wakilia kwa kukosa huduma muhimu za afya,elimu na miundombinu.

Jitihada za kututoa kwenye mstari ni kubwa sana lakini Rais Magufuli na watanzania hawatakiwi kutoka nje ya mstari.

Hulka ya mwizi ni kujitetea...Basi na sisi tuendelee kupambana naye vilivyo iwe kwa njia za kawaida au hata zile zisizo za kawaida.

Ulinzi wa Viongozi wetu uongezwe kwani kama tuna watanzania wasaliti wanaoweza kushirikiana na matapeli kufanikisha ukamataji wa mali za umma ili tu kukomoa basi ni wazi wana uwezo wa kupanga hata mapinduzi kwa kusaidiwa na watu wa nje.
 
Kuna wajinga huku badala ya kuona uchungu wa fedha tunazolipa kama FIDIA kwa mihemko yetu mijitu imebakia kumlaumu LIssu ambae ametufumbua macho namna tunavyoingizwa mikenge na watawala wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…