Msemaji wa Serikali akiri ndege mpya ya Bombardier Q 400-Dash 8 kushikiliwa nchini Canada. Awatupia lawama wanasiasa...

Hii serikali ni hovyo sana, yaani unaandika kabisa eti mwanzo serikali ilikuwa "inahisi" na sasa inahakika. Aisee serikali inatoa majibu mepesi kwa jambo linalofikirisha hii kweli ni serikali ya hisia.
 
Upinzani utoe solution kwa Serikali ipi..?? Serikali hii inayotaka kuhakikisha upinzani unakufa, Serikali hii inayonyanya Wapinzani kila siku, Serikali hii ambayo haitaki kusikia kitu kinaitwa upinzani..

Hebu wacha utani
You don't have to give them the room to shut you down on point that you are only blaming them without offering solution
 
Awamu ya tano imewafutia hoja kabisa wapinzani.

Ni aibu na nadhani tunachekwa hata na majirani zetu kubaki tunajadili swala la madeni.

kwa ulimwengu wa sasa ni aghalab sana kukuta nchi isiyo na madeni.

Sijawahi kusikia madeni yamewahi kuwa kosa popote.

Marekani yenyewe anadeni la trilioni za dola kwa china; na bado wanaendelea na maisha hutasikia wakipoteza muda kama sisi.

Njooni na hoja mbadala za changamoto tunazokumbana nazo kama Taifa ila sio hivi vioja vya madeni.

America owes China $1tn. That’s a problem for Beijing, and Trump knows it

Hoja sio deni bali chanzo na aina ya deni. Mbona mgumu kuelewa?
 
4357fe6565561619f16c799882f77f17.jpg

Na Mwandishi Wetu.

Kitendo cha Mwanasiasa na Mbunge wa Ikungi kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa Chama hicho Tundu Lissu kuishambulia serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na hivi karibuni kuihusisha na kile alichokiita kukwama kwa ndege zilizonunuliwa na serikali ya Tanzania nchini Canada kimemfanya mbunge huyo kupuuzwa na watu makini huku akihusishwa na kufilisika kisiasa.

Akiongea na Gazeti hili Kaimu Mkurugenzi wa muungano wa Taasisi zinazojihusisha na masuala ya utetezi wa Rasilimali, Haki na Utawala wa Sheria uoutwa ULINGO WA KATIBA Bwana Ally Bushiri amesema hakutarajia kuona kama maneno anayoyasikia yangeweza kutamkwa na mwanasiasa huyo aliyejipambanisha kama mtetezi wa wanyonge na mzalendo.

‘’huwezi kujiita Mzalendo ama mtetezi wa wanyonge halafu ushiriki kuihujumu serikali, hata kama inaongozwa na kiongozi usiyempenda kiasi gani, haiwezekani’’. Alisema Bushiri

‘’kila siku Lissu anaibuka na kashfa mpya, na kashfa zote ni kumchafua Rais tu, hata kama anajiandaa kugombea Urais 2020 lakini si kwa mtindo huu….Lissu lazima afahamu kwamba Waziri yeyote yule hapa Tanzania, Afrika na Duniani hana Mamlaka ya Kusaini Mkataba wa kizabuni kama ujenzi, na ndio maana kunakuwa na mamlaka za manunuzi ambazo ni huru na haziingiliwi na taasisi yoyote, na ndio maana Lowassa alipojaribu kuingilia kwenye zabuni ya Richmond alikwenda na Maji’’. Alisisitiza bwana Ally.

Aidha mkurugenzi huyo ameongeza kuwa haikuwa rahisi na isingewezekana kwa kile alichokisema Lissu kuwa Rais Magufuli alipokuwa waziri aliweza kuvunja mkataba na kampuni moja ya kigeni jambo ambalo kisheria waziri hana mamlaka ya kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba yeye si sehemu ya mkataba wa ujenzi ambayo kwa barabara kubwa hapa nchini husimamiwa na Wakala wa Barabara nchini maarufu kama TANROADS.

‘’Lissu angeweza kusema kuwa sisi kama nchi tunadaiwa, na mmoja kati ya wadeni wetu amekosa uvumilivu ameamua kuchukua hatua kali zaidi, wala haina maana ya ziada kusema tunadaiwa deni lililosababishwa na Fulani, serikali haifanyagi kazi namna hiyo dunia nzima, labda wao Chadema kama ndivyo wanavyoongozana hivyo’’. Alisisitiza

Bushiri aliongeza kuwa Tanzania kwa mujibu wa taarifa za kifedha mpaka sasa inadaiwa zaidi ya Trilioni 40 na kwamba haijaanza kukopa leo wala jana na kamwe haiwezi kuacha kukopa kesho wala kesho kutwa kwa kuwa inafuata taratibu zote za kisheria na kifedha.

‘’Mwalimu Nyerere alikopa na akadaiwa, Mzee Mwinyi naye kakopa, Rais Mkapa alikopa na akadaiwa, Mzee Kikwete naye Kadharika, na wote hawa walikopa na kulipa na kukopa na hata Magufuli amekopa na atalipa na atakopa, sasa shida iko wapi?...Mbona Marekani wanadaiwa, Uingereza Wanadaiwa..nchi zote unazozijua kubwa kwa ndogo hapa uniani zinadaiwa. Alisisitiza

Aidha bwana Bushiri amewataka watanzania kutomkubalia na kumuamini Lissu kwa haraka bila kupima jambo analowaambia kutokana na ukweli kwamba mwanasiasa huyo hachelewi kugeuka na kubadili msimamo wake bila kujali jana amesema nini.

‘’Lissu sio wa kumuamini sana. Leo anaweza kusema hivi kesho vile, ni mjanja mjanja, ndio maana mwaka 2007 Lissu alituambia watanzania tumchukie Lowassa kwa kuwa ni FISADI lakini mwaka 2015 akatuambia tumchague Lowassa kuwa Rais wa Tanzania vinginevyo tuthibitishe UFISADI wa Lowassa…hivyo anaweza siku moja akatuambia tuthibitishe haya anayoyaropoka leo…ili umuamini Lissu inakubidi uwe na akili kama zake ’’. amenukuliwa Bushiri

Hivi karibuni serikali imetoa tamko na kueleza kuwa baadhi ya wanasiasa wapo katika mkakati wa kuhujumu mipango ya maendeleo na usalama wa nchi ambao wameshiriki kuchochea kuwekwa zuio la ndege mpya ya kuwasili nchini.

Jamvi la Habari limepata taarifa ya serikali iliyosema kuwa licha ya uwepo wa zuio hilo, hatua za kidiplomasia na za kisheria zimeanza kuchukuliwa ili kulimaliza na ndege hiyo itawasili nchini.

Zuio hilo la mahakama linalodaiwa kuwekwa na kampuni moja ya ujenzi nchini Canada, ikiidai serikali fedha kufuatia kuvunjwa mkataba wa ujenzi wa moja ya barabara iliyokuwa ikijengwa nchini.

Hatua hiyo iliyochochewa na wanasiasa wanaoendeleza hujuma dhidi ya maendeleo ya nchi, imesababisha ndege ya tatu aina ya Bombardier Q 400, kuzuiwa nchini Canada.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa , Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaiadizi wa Idara ya Habari-Maelezo, Zamaradi Kawawa, alisema serikali inawaomba Watanzania kutokuwa na wasiwasi kuhusu suala hilo.

Alisema serikali ilikuwa na fununu kwamba kuna baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa, wanaendeleza juhudi za kuhujumu jitihada za Rais Dk. John Magufuli, za kuwaletea Watanzania hasa wanyonge maendeleo.

“Walikwenda kufungua madai kuwa, serikali inadaiwa na kwamba ndege hiyo ishikiliwe, watu hawa hawana uhalali wowote wa kufanya hivyo, na ni matapeli ambao wamesukumwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa wasioitakia mema nchi.''alisema

Aliongeza kuwa “Kwa kuwa serikali ilishapata fununu kwamba kuna baadhi ya viongozi wa chama cha siasa wanampango huo, sasa watu hao wamejiridhisha hadharani, kwamba wao ndio wako nyuma ya pazia la kuhujumu jitihada za serikali kwa maslahi yao ya kisiasa,” alifafanua.

Kwa mujibu wa Zamaradi alisema serikali ya Dk. Magufuli itawahakikishia Watanzania kuwa, ndege itakuja na wanaokwamisha jitihada hizo watapanda ndege hizo na ndugu zao na wafuasi wao.

Zamaradi alibainisha kuwa, kundi hilo limekuwa likichochea wafadhili wasitishe misaada nchini, wakidhani kufanya hivyo ni kukomoa serikali.

Aliongeza kuwa pia serikali inafununu kwamba watu hao wanaohujumu jitihada za kimaendeleo, wanahujumu hata hali ya usalama wa raia, hivyo inaendelea kufuatilia kwa makini.

“Tunachojifunza kama serikali, hivi misaada isipotolewa anayekomolewa ni Rais Dk. Magufuli?. Au ni Watanzania wanyonge ambao wangekosa dawa, huduma za maji na umeme.

Aliongeza “Lakutia faraja ni kwamba pamoja na jitihada hizo, washirika wa maendeleo wameongeza kasi ya ushirikiano na serikali inayoongozwa na Rais Dk. Magufuli,”.

Alisema yeyote mwenye uchungu na nchi yake angepambana ili jambo linalohusu maslahi ya taifa, likiwemo la kununua ndege lisikamwe na kama kuna mkwamo, ashiriki kukwamua badala ya kushabikia.

Kauli ya Kaimu Mkurugezi huyo wa Maelezo, imefanana na kauli mbalimbali za wananchi, walioeleza kuwa Lissu amekuwa akipotosha mambo mengi, na umefika wakati wa kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Jacob Agustino, ambaye ni mkazi Temeke Mtongani, alisema huyu mtu anapaswa kuangaliwa kwa umakini mkubwa hasa kutokana na kujifanya anajua sheria na mwisho wa siku anafanya mambo mengi ya ovyo.

Alisema kuna wakati alikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Tanzania yote ijue kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ni fisadia namba moja nchini na badala ya siku amekuwa mstari wa mbele katika kumsifia na kumfanya aonekane ni mtu safi.

"Watanzania tuweni makini, serikali inafanya kazi nzuri chini ya Rais Dk. John Magufuli,ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kila linalofanywa linafanywa kwa maslahi ya umma,''alisema.

Hivyo, alisema kila mwananchi mpenda maslahi anapaswa kuwa pamoja na Rais Dk. Magufuli kwa kuwa katika kipindi kifupi ameipa hadhi nchi kuwa na ndege zake zenyewe na hatimaye kuwa na mafanikio katika usafiri wa anga.

JAMVI LA HABARI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BAADHI ya wasomi nchini wamehoji uzalendo wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu wa kushabikia matatizo ya nchi yake badala ya kuwa sehemu ya kutafuta ufumbuzi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Profesa Benson Bana ameelezea kitendo cha Lissu kujitokeza mbele yalezea kwa mbwembwe suala la kuzuiliwa kwa ndege ya Tanzania nchini Canada, ni kitendo kinachozua maswali mengi juu ya uzalendo wake kwa Tanzania.

“Nilipomuona amejitokeza katika vyombo vya habari ilinishtua kwa sababu tangu mwanzo Lissu na wenzake walikuwa wanapinga ujio wa hata zile ndege mbili za mwanzo,” alieleza Profesa Bana. Alieleza kuwa mwenendo ambao Lissu ameendelea kuuonesha, unaashiria kuna walakini mkubwa katika suala la uzalendo na pia kujenga hisia kwamba inawezekana kuna jambo nyuma ya pazia, linalomsukuma kufanya mambo yanayoharibu maslahi ya Taifa.

Msomi huyo alisema hivi sasa kumekuwa na minong’ono mingi juu ya uzalendo wa Lissu na namna anavyosemekana kushirikiana na watu wa nje katika kuiumiza nchi. “Tuliosoma somo la Uraia tulifundishwa namna ya kuipenda nchi yako na kutumia uwezo wako kuisaidia nchi yako badala ya kuivua nguo,” alisitiza Profesa Bana huku akimfananisha mwanasiasa huyo na askari aliyoko vitani, anayeuza siri za jeshi badala ya kupambana kulisaidia jeshi lake kushinda vita.

Aidha, alieleza pia kutokufurahishwa na kitendo cha Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACTWazalendo) cha kumuuliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kupitia akaunti ya tweeter kuhusu kutokuwasili kwa ndege ya Bombardier Q400-Dash 8, ambapo Profesa Bana ameielezea njia hiyo ya mawasiliano kama si sahihi na badala yake angeweza njia ambayo si ya kila mtu kujua.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Wakili Dk Damas Ndumbaro amemuelezea Lissu kama mtu anayetafuta umaarufu kwa njia yoyote ile hata kama njia anayoitumia itakuwa na madhara kwa maslahi ya nchi.

“Haya tunayoyaona kwa Lissu inatuonesha jinsi gani upeo wake upo kiuanaharakati zaidi kuliko uongozi na katika hili ni kama bomu linalosubiri kulipuka ambalo hata viongozi wa chama chake na hata wafuasi wake wanashindwa kuling’amua,” alieleza Dk Ndumbaro. Maneno ya Dk Ndumbaro yaliungwa mkono ya Mhadhiri mwingine wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Haji Semboja ambaye alisema tatizo kubwa la Lissu ni kukosa maarifa ya uongozi.

“Lissu hajui uongozi na hii ndiyo shida kubwa inayomkabili. Hajui suala la maslahi ya nchi katika siku zijazo na siku zote amekuwa akiona mabaya,” alieleza Profesa Semboja. Kwa upande wake, mtaalamu wa sheria za kodi ya madini, Dk Hellen Kihunsi alisema hata kama kuzuiwa kwa ndege ni suala la kisheria lakini Tundu Lissu alipaswa kutumia njia bora zaidi ya kuwasilisha kwa mamlaka husika badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari.

“Masuala kama haya yana maslahi kwa Taifa mbapo hata yeye (Lissu) ni sehemu ya Taifa hili, lakini kwa mwenendo ambao siku zote amekuwa akiuonesha unatilia shaka uadilifu na uzalendo wake kwa Taifa,” alieleza Dk Kihunsi. Tangu Serikali ya Awamu ya Tano ianze kuchukua juhudi ya kuifufua Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), kumekuwa na baadhi ya wanasiasa kutoka vyama vya upinzani wakipinga juhudi hizo, ambapo ndege mbili za awali aina ya Bombardier zilipigiwa kelele na wapinzani wakidai hazifai licha ya kwamba zimekuwa msaada mkubwa katika sekta ya usafirishaji.
 
Narudia kusema tena,
Msukuma akija mjini bila KUJIPANGA lazima awe TAPELI.
fuatilia hili.
 
4357fe6565561619f16c799882f77f17.jpg

Na Mwandishi Wetu.

Kitendo cha Mwanasiasa na Mbunge wa Ikungi kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa Chama hicho Tundu Lissu kuishambulia serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na hivi karibuni kuihusisha na kile alichokiita kukwama kwa ndege zilizonunuliwa na serikali ya Tanzania nchini Canada kimemfanya mbunge huyo kupuuzwa na watu makini huku akihusishwa na kufilisika kisiasa.

Akiongea na Gazeti hili Kaimu Mkurugenzi wa muungano wa Taasisi zinazojihusisha na masuala ya utetezi wa Rasilimali, Haki na Utawala wa Sheria uoutwa ULINGO WA KATIBA Bwana Ally Bushiri amesema hakutarajia kuona kama maneno anayoyasikia yangeweza kutamkwa na mwanasiasa huyo aliyejipambanisha kama mtetezi wa wanyonge na mzalendo.

‘’huwezi kujiita Mzalendo ama mtetezi wa wanyonge halafu ushiriki kuihujumu serikali, hata kama inaongozwa na kiongozi usiyempenda kiasi gani, haiwezekani’’. Alisema Bushiri

‘’kila siku Lissu anaibuka na kashfa mpya, na kashfa zote ni kumchafua Rais tu, hata kama anajiandaa kugombea Urais 2020 lakini si kwa mtindo huu….Lissu lazima afahamu kwamba Waziri yeyote yule hapa Tanzania, Afrika na Duniani hana Mamlaka ya Kusaini Mkataba wa kizabuni kama ujenzi, na ndio maana kunakuwa na mamlaka za manunuzi ambazo ni huru na haziingiliwi na taasisi yoyote, na ndio maana Lowassa alipojaribu kuingilia kwenye zabuni ya Richmond alikwenda na Maji’’. Alisisitiza bwana Ally.

Aidha mkurugenzi huyo ameongeza kuwa haikuwa rahisi na isingewezekana kwa kile alichokisema Lissu kuwa Rais Magufuli alipokuwa waziri aliweza kuvunja mkataba na kampuni moja ya kigeni jambo ambalo kisheria waziri hana mamlaka ya kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba yeye si sehemu ya mkataba wa ujenzi ambayo kwa barabara kubwa hapa nchini husimamiwa na Wakala wa Barabara nchini maarufu kama TANROADS.

‘’Lissu angeweza kusema kuwa sisi kama nchi tunadaiwa, na mmoja kati ya wadeni wetu amekosa uvumilivu ameamua kuchukua hatua kali zaidi, wala haina maana ya ziada kusema tunadaiwa deni lililosababishwa na Fulani, serikali haifanyagi kazi namna hiyo dunia nzima, labda wao Chadema kama ndivyo wanavyoongozana hivyo’’. Alisisitiza

Bushiri aliongeza kuwa Tanzania kwa mujibu wa taarifa za kifedha mpaka sasa inadaiwa zaidi ya Trilioni 40 na kwamba haijaanza kukopa leo wala jana na kamwe haiwezi kuacha kukopa kesho wala kesho kutwa kwa kuwa inafuata taratibu zote za kisheria na kifedha.

‘’Mwalimu Nyerere alikopa na akadaiwa, Mzee Mwinyi naye kakopa, Rais Mkapa alikopa na akadaiwa, Mzee Kikwete naye Kadharika, na wote hawa walikopa na kulipa na kukopa na hata Magufuli amekopa na atalipa na atakopa, sasa shida iko wapi?...Mbona Marekani wanadaiwa, Uingereza Wanadaiwa..nchi zote unazozijua kubwa kwa ndogo hapa uniani zinadaiwa. Alisisitiza

Aidha bwana Bushiri amewataka watanzania kutomkubalia na kumuamini Lissu kwa haraka bila kupima jambo analowaambia kutokana na ukweli kwamba mwanasiasa huyo hachelewi kugeuka na kubadili msimamo wake bila kujali jana amesema nini.

‘’Lissu sio wa kumuamini sana. Leo anaweza kusema hivi kesho vile, ni mjanja mjanja, ndio maana mwaka 2007 Lissu alituambia watanzania tumchukie Lowassa kwa kuwa ni FISADI lakini mwaka 2015 akatuambia tumchague Lowassa kuwa Rais wa Tanzania vinginevyo tuthibitishe UFISADI wa Lowassa…hivyo anaweza siku moja akatuambia tuthibitishe haya anayoyaropoka leo…ili umuamini Lissu inakubidi uwe na akili kama zake ’’. amenukuliwa Bushiri

Hivi karibuni serikali imetoa tamko na kueleza kuwa baadhi ya wanasiasa wapo katika mkakati wa kuhujumu mipango ya maendeleo na usalama wa nchi ambao wameshiriki kuchochea kuwekwa zuio la ndege mpya ya kuwasili nchini.

Jamvi la Habari limepata taarifa ya serikali iliyosema kuwa licha ya uwepo wa zuio hilo, hatua za kidiplomasia na za kisheria zimeanza kuchukuliwa ili kulimaliza na ndege hiyo itawasili nchini.

Zuio hilo la mahakama linalodaiwa kuwekwa na kampuni moja ya ujenzi nchini Canada, ikiidai serikali fedha kufuatia kuvunjwa mkataba wa ujenzi wa moja ya barabara iliyokuwa ikijengwa nchini.

Hatua hiyo iliyochochewa na wanasiasa wanaoendeleza hujuma dhidi ya maendeleo ya nchi, imesababisha ndege ya tatu aina ya Bombardier Q 400, kuzuiwa nchini Canada.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa , Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaiadizi wa Idara ya Habari-Maelezo, Zamaradi Kawawa, alisema serikali inawaomba Watanzania kutokuwa na wasiwasi kuhusu suala hilo.

Alisema serikali ilikuwa na fununu kwamba kuna baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa, wanaendeleza juhudi za kuhujumu jitihada za Rais Dk. John Magufuli, za kuwaletea Watanzania hasa wanyonge maendeleo.

“Walikwenda kufungua madai kuwa, serikali inadaiwa na kwamba ndege hiyo ishikiliwe, watu hawa hawana uhalali wowote wa kufanya hivyo, na ni matapeli ambao wamesukumwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa wasioitakia mema nchi.''alisema

Aliongeza kuwa “Kwa kuwa serikali ilishapata fununu kwamba kuna baadhi ya viongozi wa chama cha siasa wanampango huo, sasa watu hao wamejiridhisha hadharani, kwamba wao ndio wako nyuma ya pazia la kuhujumu jitihada za serikali kwa maslahi yao ya kisiasa,” alifafanua.

Kwa mujibu wa Zamaradi alisema serikali ya Dk. Magufuli itawahakikishia Watanzania kuwa, ndege itakuja na wanaokwamisha jitihada hizo watapanda ndege hizo na ndugu zao na wafuasi wao.

Zamaradi alibainisha kuwa, kundi hilo limekuwa likichochea wafadhili wasitishe misaada nchini, wakidhani kufanya hivyo ni kukomoa serikali.

Aliongeza kuwa pia serikali inafununu kwamba watu hao wanaohujumu jitihada za kimaendeleo, wanahujumu hata hali ya usalama wa raia, hivyo inaendelea kufuatilia kwa makini.

“Tunachojifunza kama serikali, hivi misaada isipotolewa anayekomolewa ni Rais Dk. Magufuli?. Au ni Watanzania wanyonge ambao wangekosa dawa, huduma za maji na umeme.

Aliongeza “Lakutia faraja ni kwamba pamoja na jitihada hizo, washirika wa maendeleo wameongeza kasi ya ushirikiano na serikali inayoongozwa na Rais Dk. Magufuli,”.

Alisema yeyote mwenye uchungu na nchi yake angepambana ili jambo linalohusu maslahi ya taifa, likiwemo la kununua ndege lisikamwe na kama kuna mkwamo, ashiriki kukwamua badala ya kushabikia.

Kauli ya Kaimu Mkurugezi huyo wa Maelezo, imefanana na kauli mbalimbali za wananchi, walioeleza kuwa Lissu amekuwa akipotosha mambo mengi, na umefika wakati wa kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Jacob Agustino, ambaye ni mkazi Temeke Mtongani, alisema huyu mtu anapaswa kuangaliwa kwa umakini mkubwa hasa kutokana na kujifanya anajua sheria na mwisho wa siku anafanya mambo mengi ya ovyo.

Alisema kuna wakati alikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Tanzania yote ijue kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ni fisadia namba moja nchini na badala ya siku amekuwa mstari wa mbele katika kumsifia na kumfanya aonekane ni mtu safi.

"Watanzania tuweni makini, serikali inafanya kazi nzuri chini ya Rais Dk. John Magufuli,ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kila linalofanywa linafanywa kwa maslahi ya umma,''alisema.

Hivyo, alisema kila mwananchi mpenda maslahi anapaswa kuwa pamoja na Rais Dk. Magufuli kwa kuwa katika kipindi kifupi ameipa hadhi nchi kuwa na ndege zake zenyewe na hatimaye kuwa na mafanikio katika usafiri wa anga.

JAMVI LA HABARI

Sent using Jamii Forums mobile app
hivi cerebrum yako inafanya kazi kweli, sijui umeongea nini,
 
Akiongea na Gazeti hili Kaimu Mkurugenzi wa muungano wa Taasisi zinazojihusisha na masuala ya utetezi wa Rasilimali, Haki na Utawala wa Sheria uoutwa ULINGO WA KATIBA Bwana Ally Bushiri amesema hakutarajia kuona kama maneno anayoyasikia yangeweza kutamkwa na mwanasiasa huyo aliyejipambanisha kama mtetezi wa wanyonge na mzalendo.
Huyu kwani ni msemaji wa serikali? Hayo ni maoni yake binafsi kama anataka ajibu hoja za Lissu kwa vielelezo siyo kwa porojo. Kazi ya upinzani wa nchi yoyote ni kuikosoa serikali tawala dhidi ya mambo mbali mbali yanayoonekana kutokwenda sawa. Siyo kutokuwa na uzalendo kama kama huyu jamaa na wengine wanavyofikiri.
 
Mazuzu wa lumumba akili zao fupi mno nyie badala ya kutafuta namna ya kulipa deni ndio kwanza mnatafuta mchawi

Mwambieni babu yenu kuongoza nchi kwahitaji hekima ya mungu
 
Back
Top Bottom