Nimefuatilia sana hii issue... jamaa ka-trend ile mbaya!
Kama u-Tanzania wake ni uzushi basi itakuwa tunamuonea Msigwa kwa sababu, nimefuatilia sana hii habari! Wakati habari ya Msigwa, as of now, imekuwa posted Twitter 20 hours ago, Al Jazeera walitoa habari yao saa 24 zilizopita na wamemtaja kama Mtanzania.
New York Times, wao wanaonekana waliandika mapema zaidi, nao wamemtambulisha kama Mtanzania!!!
Media karibu zote kubwanchini UK , including Reuters, BBC, na The Economist ambazo ni za UK; wote hawa wamemtaja kama Mtanzania!!
Of course, The Guardian (UK) hawajamtaja kama Mtanzania bali wamemtaja kama "Zanzibari"!
Sijaona source HATA MOJA iliyomtaja kwamba ni Mwingereza!!
Hata zile ambazo hazikusema kwamba ni Mtanzania, ziliishia tu kusema "born in Zanzibar, based in UK", na source hizi ikiwa ni pamoja na Kent University alikozeekea!!
Hata wakati anatangazwa, aliyetaja jina hakusema ni Mwingereza bali "born in Zanzibar, active in UK"!
So, sitaki kuamini kwamba wote hao source yao ni Gerson Msigwa!!!
Na Wachangiaji wengine hapa wanadai katoka ZNZ kabla ya Muungano, na kwahiyo haiwezi kuwa Mtanzania!!!
Hapa sources nyingi zinaonesha "alikimbia" ZNZ mwishoni mwa 1960's!! Sources hizo ni pamoja na Kent University!!
Source pekee ambayo inaweza kuendana na hayo madai, ni New York Times ambao wameandika "
Then, in 1964, a violent uprising forced Gurnah, at age 18, to flee to England." Hata hivyo, source zote zinasema amezaliwa 1948, na kwahiyo kama alikimbilia UK at the age of 18, ina maana alishakuwa Mtanzania!!
Hata hivyo, sources nyingi zinasema Mwamba alimbilia UK akiwa 20 years!! Na tukiacha hizi hypes za sasa, back 2001, The Guardian UK liliandika
In 1969, a young African fled persecution in Zanzibar for what he envisaged as freedom in Britain. Here, the novelist recalls what he found and reflects on what has happened in the years since.
Hayo yalikuwa ni mahojiano kati ya The Guardian na Abdulrazak Gurnah!! Na katika mahojiano hayo, The Guardian wanamnukuu Mwamba akisema"-
I arrived in Britain at around the same time, although I wasn't Asian. I came from Zanzibar, a small island off Africa which in 1964 had seen a violent uprising that led to catastrophic upheaval. Thousands were slaughtered, whole communities were expelled and many hundreds imprisoned. In the shambles and persecutions that followed, a vindictive terror ruled our lives. At 18, the year after I finished school, I escaped. Many others did the same; some were captured and disappeared, most got safely away.
Of course, ni contradicting kwa sababu kama alizaliwa 1948, na kwamba alitoroka when he was 18, it means it's 1966 and not 1969 as said above!!
Lakini makala/ripoti inaanza kwa kusema:-
They didn't call it asylum then. The phrase was illegal immigrant. When I came to England in the late 60s, Sergeant Pepper was ruling the land, de Gaulle was the Great Satan and it was only months before Enoch Powell made his classical allusion to the Tiber.
Sentensi hiyo inaendana na 1969, na kwahiyo sina shaka Dully aliondoka ZNZ wakati tayari akiwa Mtanzania!! That having been said, tuachieni Mtanzania mwenzetu, na kama hamtaki, juzi tu hapa mmekopeshwa Mtanzania mwingine aitwae Kibu Denis... mchukueni huyo ambae, Haji Manara amempa kabila la Makonde!!
But wait... mbona incontinency kwenye hiyo miaka?
Hebu waungwana naomba mnijuze....
Ule unyanyama wa during and after revolution kule ZNZ uliendelea hadi mwishoni mwa 1960's especially kwa watu ambao hawakuwa Politicians kama ilivyokuwa Braza Dully?!!
Sijui kwanini nahisi Babu Dully na yeye alikuwa mjanja mjanja tu kama Watanzania wengine kwa kuamua kujilipua hadi kwa Malkia kwa gia ya ukimbizi!! I know, by the time, Mzee Karume alikuwa Mafia kweli kweli kwa Wanasiasa Wasomi lakini kwa kavulana ka miaka 18-20?! Haya bhana....
Sema kama Babu Dully kama anajitangaza mwenyewe na kujiona ni Mtanzania, akitaka kujua kama kweli yeye ni Mtanzania basi autangazie ulimwengu kwamba "
...hatimae nimeamua kurudi nyumbani kugombea urais ama wa ZNZ au Tanzania" kisha baada ya hapo aanze kutembelea pages za Msigwa na za Uhamiaji
Nachoipendea nchi yangu, wale wanaokupigia matarumbeta hii leo ndio watakaotangaza wewe sio Mtanzania na wale ambao leo wanasema wewe sio Mtanzania, ndio hao hao watakaosema "wewe ni Mtanzania swafi..."