Aliingia uingereza kwa kutumia visa ya utalii ( tourist visa). Baada ya kupata shule alibadilisha visa yake kuwa ya uanafunzi na baadae akachukua uraia. Baada ya Muungano wa mwaka 1964 wazanzibari wote walikuwa raia wa Tanzania. Ni dhahiri huyu bwana alitumia paspoti ya Tanzania alipoomba visa. Uraia huo wa Zanzibar uliacha kutambulika nje ya mipaka ya JMT baada ya Muungano. Hata ndani ya mipaka ishara ya uraia ni vitambulisho vya ukaazi na sio paspoti.
Usiyejua maana ya protectorate ni wewe. Baada ya mkataba wa Heligoland- Zanzibar, waingereza waliigeuza Zanzibar kuwa protectorate yao na kumfanya Hamoud bin Mohammed kuwa Sultan wa Zanzibar baada ya kumpiga Khalid bin Bhargash. Kwa kifupi Sultan alikuwa figure head lakini watawala walikuwa waingereza. Walipochoka, mwaka 1963 wakamrudishia utawala Sultan Jamshid.
Unajidanganya sana unapofikiri kuwa machogo tuna uchu na Zanzibar. Wengi wetu hatujawahi kufika wala kutamani kufika Zanzibar. Matatizo mliyonayo ni ya kwenu wenyewe kwa sababu hamjawahi kupendana. Mfano ni huyu Gurnah, wakati dunia nzima inampongeza kama mwafrika na yeye mwenyewe kusema kuwa hiyo zawadi ni kwa ajili ya waafrika na Afrika, nyinyi mnakazania kuwa ni mOmani na Muarabu! Hata haya hamna.
Amandla....