Msemaji wa Serikali umedanganya; tuzo ya Nobel haijaenda kwa Raia wa Tanzania

Siku zote walikua wapi kumtaja??

Awamu iliyopita waliaminishwa mtu yoyote aliyepo nje ya Tanzania ni kibaraka wa mabeberu na hana nia njema na Tanzania
 
Excuse my language Mkuu kwa hiyo Zitto na yule marehemu walikuwa wanamla tigo huyo jamaa?
Hahahaha
Yasemekana hata Msemaji wa Chama cha Sufiani Kwa SASA na yeye ni Kama Sufiani
 
Pengine wameruhusu dual citizenship!

View attachment 1967578
Sasa huyu hakuwahi kuwa raia wa tanganyika au tanzania maana raia wa tanzania ni wale raia wote waliokuwepo tanganyika na zanzibar april 26. Huyu ameondoka mwaka 1960 kipindi hiko zanzkbar ilikua chini ya wauza watumwa wenye asili ya kiarabu na tanganyika chini ya wauza watumwa wa kutokea ulaya
 
Hivi si alitumbuliwa ikawaje akabaki tena nafasi yake kuna mtu alichaguliwa
 
Walivyo na memory chip ndogo wamesahau kwamba Tanzania Haina Uraia pacha![emoji2956] Gumah sio Mtanzania ni Mwingereza mwenye asili ya Tanzania hususani Zanzibar
 
Mdesi sana huyo mbena manga. Agaya luhala mpuva
 
Utalii gani huo anaufanya kwa miaka 52 mpaka sasa? Unajua maana ya protectorate? Na ni lini aliukana uraia wake wa Zanzibari wake mpaka umwite Mtanzania? Tatizo lako wewe unamiini propaganda, hadithi ulizolishwa na watu waliokuwa na uchu na Zanzibar kwa muda mrefu.
 
Aliingia uingereza kwa kutumia visa ya utalii ( tourist visa). Baada ya kupata shule alibadilisha visa yake kuwa ya uanafunzi na baadae akachukua uraia. Baada ya Muungano wa mwaka 1964 wazanzibari wote walikuwa raia wa Tanzania. Ni dhahiri huyu bwana alitumia paspoti ya Tanzania alipoomba visa. Uraia huo wa Zanzibar uliacha kutambulika nje ya mipaka ya JMT baada ya Muungano. Hata ndani ya mipaka ishara ya uraia ni vitambulisho vya ukaazi na sio paspoti.

Usiyejua maana ya protectorate ni wewe. Baada ya mkataba wa Heligoland- Zanzibar, waingereza waliigeuza Zanzibar kuwa protectorate yao na kumfanya Hamoud bin Mohammed kuwa Sultan wa Zanzibar baada ya kumpiga Khalid bin Bhargash. Kwa kifupi Sultan alikuwa figure head lakini watawala walikuwa waingereza. Walipochoka, mwaka 1963 wakamrudishia utawala Sultan Jamshid.

Unajidanganya sana unapofikiri kuwa machogo tuna uchu na Zanzibar. Wengi wetu hatujawahi kufika wala kutamani kufika Zanzibar. Matatizo mliyonayo ni ya kwenu wenyewe kwa sababu hamjawahi kupendana. Mfano ni huyu Gurnah, wakati dunia nzima inampongeza kama mwafrika na yeye mwenyewe kusema kuwa hiyo zawadi ni kwa ajili ya waafrika na Afrika, nyinyi mnakazania kuwa ni mOmani na Muarabu! Hata haya hamna.

Amandla....
 
Hakuna mtalii wa kuishi miaka 52 utaliini. Huyo alikuwa ni mkimbizi wa mapinduzi haramu na kama ubalozi wa Uingereza ungekuwa na visa rasmi ya wakimbizi wa mapinduzi haramu angeiomba hiyo badala ya visa ya utalii. Sema wewe na wenzako wenye mawazo kama yako ndiyo mliacha kuitambua Zanzibar mwaka 1964. Siyo watu wote.

Protectorate ni chombo tuu cha sheria tena unaweza kusema ni chombo cha imperialism. Haina sovereignity yoyote na wala haitambuliki kwa watu wenye akili. Na huwezi kusema Zanzibar ni sehemu ya Britain, kihistoria Zanzibar ilikuwa ni sehemu ya Oman.

Kwa taarifa yako basi, Nyerere alikuwa na mpango wa kuimeza Zanzibar tangu miaka ya 1956. Kwa nini unafikiri Nyerere alikaa kimya wakati Kambona anapeleka silaha za kuleta mapinduzi haramu Zanzibar? Unafikiri alikuwa hajui kinachopangwa kufanywa?
 
Aisee... Kwa hiyo hutaki hizo sifa za Nobelist tena??
 
Hatuna huo muda mkuu kwa maana watanzania tunaowajua huwa hawafuatilii habari wakishaambiwa. wakiambiwa Mike Tyson ni mtoto wa mzee Wassira utakuta ndio habari iliyozagaa kila mtaa...
[emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],we jamaa umetishs[emoji23][emoji23]
 
CCM ni wanafiki wa kiwango cha PHD. Hamza alikuwa mwanachama na mfadhili wao wamemkataa. Leo wanajipendekeza kwa raia wa Uingereza kisa amepata Nobel Prize!
 
Hata Tundu Lisu akipewa tuzo utashangaa Serikali ya Tanzania wana mpongeza japo kwa sasa hawataki kumuona. Na walitaka kumuua.
Huyu alie pewa hii tunzo ni Mtanzania wa kuzaliwa lakini ni raia wa Uingereza. Alitofautiana na wakubwa akahama nchi..
Kujisahaulisha na unafiki ndio jadi yetu. Wakati utaalamu wa mtanzania haithaminiki hapa nchini kwetu nje unathaminika...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…