Msemaji wa Simba SC yangu Ahmed Ally tafadhali popote pale ulipo nakuomba unijibu haya Maswali yangu....

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
63,685
Reaction score
128,178
1. Nani aliyekuambia kuwa Simba SC ikitangaza Kufungwa Mechi zake za Pre Season huko Misri ni vibaya kwa Mashabiki?

2. Kama umesema Watu wa Kitengo cha Habari Simba SC mmekubaliana msitoe Taarifa yoyote ya Matokeo ya Mechi za Pre Season huko Misri katika Page ya Simba SC ili kutowashtua Mashabiki sasa ilikuwaje na kwanini Simba SC ikifanya vyema kwa Kushinda Mechi huko haraka sana mnatupa Taarifa kupitia Page yenu?

3. Ni mwana Simba SC gani labda kakuambia kuwa Kipaumbele chetu wana Simba SC kabla ya Msimu wa Ligi Kuu kuanza na wa Mashindano mbalimbali ni kupata Maelezo mengi ya kuhusu Jezi mpya za Simba SC kutoka kwa Mdhamini wetu huyo Mtani wangu wa Kihaya?

4. Je, unajua kuwa wana Simba SC hata Wewe pia wameshakuchoka kwa tabia yako ya Kuipamba Simba SC kila mara ili Kuwatuliza wakati ukweli wanaujua kuwa Simba SC hakuko sawa?

5. Je, una uhakika kuwa Majukumu yako unayatendea Haki na kwamba hata Wasemaji wa Vilabu vikubwa duniani nao hufanya Mzaha na Utoto mbele ya Press kama ambavyo umekuwa ukifanya Wewe huku ukidhani unapatia wakati kiukweli huwa si tu Unaboa bali Unaharibu kabisa?

6. Kwahiyo uzuri wa Jezi Mpya za Simba SC za Msimu huu zilizotengenezwa nchini Italia ndiyo zitatufanya tusiwe Pombe ya Ngomani mbele ya Yanga SC kila mara tunapokutana nayo?

7. Kwanini technically tu umeshindwa Kujigawa Kiutendaji ili Wewe ubakie kama Msemaji pekee na atafutwe Mtu very competent wa kufanya Marketing mwenye both persuasive and convincing Marketing Skills ambazo Wewe huna kabisa japo unalazimisha kuwa nazo?

Nitashukuru ukinijibu.
 
Ahmed Aly taaluma yake nyingine ni comedy kwaiyo anachokifanya kwake ni kawaida wanaomzingatia ni wale aliowasema Rage!
 
Hivi Misiri kuna nini mbona wanapenda sana kwenda huko kila pre season.
Kwann wasibadili mazingira.
Hata Taifa stars alikwenda ku-camp kule kabla hajarejea.

Niliona Kaizer chiefs wao walienda Netherlands.....na walipata friendlies na timu za timu za ligi kuu za huko.

Hata Mamelodi alikuwa Spain, na alipata friendly match na Granada.
 
Ahmed Aly taaluma yake nyingine ni comedy kwaiyo anachokifanya kwake ni kawaida wanaomzingatia ni wale aliowasema Rage!
Aliowasema Rage nawe pia Ukiwemo vile vile.
 
Kwa sasa habari kuu ni jezi. Hizo mechi za kuipima zipo nyingi tu zinachezwa, siku nyingine wanacheza asubuhi na jioni. Hata muda huu ninapoandika, kuna mechi ya mazoezi Simba wanacheza
 
Haya mambo ya kuficha matokeo hata mimi wamenishangaza kdg aisee.
kwasasa hii timu ni kama wamejimilikisha watu wachache (wanachama hawana haki ya kuona maendeleo ya timu yao)
 
Mukhtari njoo umjibie kaka ako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…