Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 3,359
- 6,568
Hata ulaya ipo hivyo kwenye kila klabu huwa kuna watu ambao huwa ni vyanzo vya habari vya waandishi wa habari. We unadhani zile taarifa tunazozipata kutoka ulaya kuwa wachezaji wa timu flani hawamtaki kocha au hakuna maelewano katika dressing rooms huwa zinawafikiaje wanahabari kama sio hao whistle blowers?Ili kuusaidia mpira wetu ufike mbali tunawahitaji watu kama Jemedari wawe wengi zaidi
Kama hiki anachokiripoti kina ukweli maana yake kinaweza kuja kuwa msaada kwa wakubwa ambao walikuwa hawana hizo taarifa.
Maana yake sisi wote tunajua mifumo yetu ya kiutawala ilivyogubikwa na lundo la wapigaji huku sponsors wakiwa hawapati taarifa ya kinachoendelea.
Ni Jemedari huyu huyu aliyefanya Yanga Princess iweze kupata stahiki zake baada ya wachezaji wengi kuweka mgomo kufuatia madai yao.
Inawezekana ilikuuma na kufanya umchukie jamaa kwa kashfa ya Club kutolipa mishahara kuona kama Club yako imechafuliwa.
Lakini huangalii upande wa pili wa ndugu wa hao wachezaji ambao wako nyuma yao kama tegemezi, kuona jinsi ambavyo wanaweza kumuona jamaa kama shujaa kwa kufanya watoto zao wapate stahiki zao.
Hata ile ishu ya timu ya Majimaji kutelekezwa unafikiri bila nguvu ya watu wa media kufikishiwa za chini ya kapeti wasi expose public kilichotokea ni kivipi wangeweza kusaidiwa?
Unakumbuka mpaka Erasto Nyoni anatoa 1M kuwalipia madeni?
Unafikiri zile zilikuwa ni taarifa official zilizotolewa na Clubs au ni whistleblowers?
Unakumbuka ishu ya timu ya vijana ya Taifa? madogo waliivusha Tanzania kwenye hatua ya hadi nusu fainali ambapo walifanya nchi ipate zaidi ya sh. 190M (kama sikosei) halafu TFF ikawarudisha nyumbani na kila mtu akachukua 50,000 hapo ni plus nauli.
Halafu madogo hadi jezi walinyang'anywa.
Baada ya hizo taarifa kumfikia Jemedari na yeye kupost public kila mtu aliwashangaa TFF kwa ukatili wao.
Pengine hata wewe unayemnanga Jemedari ulikuwa ni mmoja wao waliyeshangaa kitendo hicho kilichofanywa na TFF.
Kuna uwezekano watu wa media za michezo wengi ni waoga ambao hawana guts za kufanya hiki anachofanya Jemedari ndio maana wahanga wanapokumbana na changamoto wanamtafuta yeye
Nakuhakikishia mbali na kasoro zake kama binadamu ila huyu jamaa ni msaada sana kwenye soka letu.
Wachezaji kutoka Clubs zingine wanapoona situation kama hiyo iliwahi kutokea sehemu nyingine na ikaja kuwa solved baada ya hizo taarifa kuwa exposed na media.
Na wao wanaona bora wapitie njia hiyo hiyo ili kama kuna wakwamishaji wajulikane na wao wapate stahiki zao.
Unaweza kumchukia Jemedari kwasababu zako binafsi lakini haina maana kwenye hili anakosea.
Hata Fabrizio Romano anapata habari haraka kuliko watu wengine kutokana na kuwa na hao whistleblowers ndani ya klabu mbalimbali.