OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Tunafahamu Dismas Ten ni moja wa maofisa ndani ya klabu ya Yanga. Kimsingi anaitambua mipaka yake nje na ndani ya ofisi
:
Yanga SC ni mshindani wa Simba SC kimasoko. Kila mmoja ana wajibu wa kuheshimu hatimiliki za mwenzake.
:
Kuna video imepostiwa na Ten ambayo haipo sawa kibiashara
:
➡️ Haki za Matangazo: Ten ametumia picha za Chama, akitangaza jarida la Yanga.
:
Nani amemruhusu kufanya Tangazo na mchezaji wa kampuni shindani?
:
➡️ Haki za Picha: Ten ametumia sura ya Chama, mchezaji halali wa Simba akiwa na jezi za Yanga bila ridhaa ya klabu husika
:
Je, Ten ni mwandishi wa habari? Je, kuna fair use?
:
Kimsingi hakuna fair use kwa sababu kuna commercial promo?
:
Simba wakiamua kumchukulia hatua Ten atakuwa na kesi ya kujibu. Ikumbukwe Ten ni ofisa wa Yanga na ametekeleza kosa hili akiwa kwenye shughuli zake za kila siku ndani ya klabu.
:
Je Yanga wamemchukulia hatua?
:
Kuhariri picha ya mchezaji sio kosa kama una lengo la
:
➡️ Kuhabarisha
➡️ Kutania (Fair Comment)
➡️ Matumizi yasiyo ya kibiashara (Fair use)
:
Simba wana haki ya kumshtaki kwa ajili ya "nominal damages", kwa sababu hili limezua mshtuko kwa washikadau na mashabiki wa klabu ya Simba SC.
:
Simba wana haki ya Compensatory Damages kwa Yanga SC kupitia mauzo ya hilo jarida ambalo Chama ametokea kwenye promo yake labda kama Yanga SC itamkana Ten na kumwadhibu.