Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Msemo huu nimeunyambua toka kwa msemo mashuhuri wa Bob Marley kuwa "in the abundance of water a fool is thirsty". Yaani, ukifa kwa kiu wakati unezungukwa na maji safi na salama tatizo ni upumbavu wako...yaani umeshindwa kubuni namna yoyote (hata kulamba kama mbwa) kuyafikisha maji kwenye kanwa lako.
Watu wanaililia serikali umeme na maji..watawala nao wanalia...tumeshindwaje kuvuna umeme wa jua, upepo, au mawimbi? Teknolojia ya renewable energy iko mbali sana na inayowezekana. Mji mpya wa serikali Dodoma ungeweka lengo la kutumia nishati mbadala (RE) kuliko kusubiri mabwawa yajae.
Tunaweza vipi kutengeneza mabwawa ya akiba ya maji ya mvua na mito na kuyafungulia kina cha mabwawa ya umeme kikianza kushuka? Je, tunaweza kuweka Sera katika kodi kwa makampuni na watu binafsi kutumia umeme wa jua au RE nyingine kama sehemu ya energy mixture yao? Kwa kadiri wanaongeza matumizi ya RE wanapata afueni mbalimbali za kodi, mitaji, na?
Swali fyatu kwa kwelini hili...hivi kweli Tanzania Kuna tatizo la ukosefu wa maji na nishati?
Au tumekuwa ni mpumbavu anayelalamikia kiu akiangalia ndoo ya maji safi na salama? Akiiomba serikali imtengenezee kata ya kunywea maji.
MM (Mwanakijiji Podcast Returning Soon)