Msemo wa 'afutatu' unaovuma mitandaoni chanzo chake ni kipi?

Msemo wa 'afutatu' unaovuma mitandaoni chanzo chake ni kipi?

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
12,207
Reaction score
26,521
Habari za muda huu wana Jf.

Wiki hii nikipita karibia kila mitandaoni naona msemo wa 'afutatu' unatembea sana, kwenye status, memes nk mpaka imekuwa kama upuuzi fulani.

Nimepata shauku ya kujua imeanza vipi mpaka kupata muitikio mkubwa kiasi hiki na kushika trend ya mitandao ya kibongo?

Picha za kusindikizia uzi hizo hapo chini.

ac604cc5dcae4cf89d2cb4bb6772f00a.jpg


2d086b3ea20b427fa03ee4cd1552a4b2.jpg


#UziTayari
 
Watanzania wengi ni "wasahaulifu" pia wanapenda kujadili issues zisizo na maana wala mustakabali wa maisha yao ya kila siku kwa kisingizio cha kutoa "stress"

Mfano kwa sasa mada motomoto ni ukosefu wa maji na umeme so huwa kuna watu kazi yao ni kuleta vitu kama hivyo ambavyo vitashabikiwa na wengi na hivyo kupoteza lengo kuu ya mambo la msingi yanayowakabili watu.

Hii ndio inaitwa "spinning" na watu wapo maalum kwa kazi hiyo.
 
Kifupi ni hivi'
Kuna clip inazagaa mtandaoni yaan mzee alienda mochwari kuchukua maiti alikua na AFTATU wahudumu wakamwambia ni zaidi ya MILLION...Akaanza kulia akisema amemkumbuka nyerere kama angekuepo angempa hyo maiti kwa AFTATU...

Kinachochekesha zaid alipewa juice kama kupoza maumivu,akaacha na kulia hapohapo....nenda kwenye instagram page ya ben paul ndio kapost.

Comment credit MAWEED nimesahau Uzi aliotolea ufafanuz huu
 
Back
Top Bottom