Msemo wa "D mbili" una maana gani?

Msemo wa "D mbili" una maana gani?

Watu wanaposema "kama huna D mbili" utanielewa huwa wana maana gani?

Zamani nilikuwa naona pia humu JF watu wanakomenti sana DD kwenye nyuzi pia.

Ninavyo elewa mimi ni kuwa D mbili ukiwa nazo maana yake una division 4 ile ya mwisho kabisa form 4( IV ya 33), mwenye D moja au F zote huyo anaangukia kwenye division zero.

Kwa maana hiyo msemo ‘kama una D mbili’ unamaanisha ‘kama hukupata zero form 4’ basi utaelewa kinacho maanishwa ama kama hukupata zero basi una ufahamu wa kutosha kuelewa hii ‘code’
 
Kuna VI college naskia uwe na nia tuh na ada ulipe kwa awamu
sawa ila ni ufundi yaani vinatoa level za NVA level 1 to 3
Vyuo vya kati vinatoa kuanzia NTA 4 (Certificate) to NTA 6 (diploma)
Hivi vigezo vimewekwa na NACTVET
 
Ukifeli shule ukitaka kusomeshwa swali la kwanza unaulizwa katika masomo yote uliofeli una "D MBILI" ili atleast tukuendeleze kielimu mana kila Profession inataka uwe na D mbili!
Kwahiyo imekua famous kwa style hio!
Kwamba Kama Huna D Mbili huwezi kuelewa jambo manake wewe ni mbumbumbu kabisa!
Umetisha Sana
 
D mbili ni minimum pass marks. Wanamaanisha kama kidato cha nne huna D mbili basi una uwezo mdogo wa kiakili hivo hakuna jambo utaelewa
Hii imetokana na matangazo ya vyuo vya kati kutaka D mbili kwa masomo yasiyo ya Dini ili kupata admission
Siyo D 3 tena siku hizi?
 
F F F F F F F = DIVISION ZERO
F F F F F F D = DIVISION ZERO
F F F F F D D = DIV FOUR.

Umeelewa umuhimu wa D mbili?

ZERO ni FAILURE haupati CHETI.

Kuanzia DIV FOUR - UMEFAULU na unapewa CHETI cha UFAULU.

Na pia inabidi tuanzishe msemo mwingine wa lazima UWE NA C TATU.
 
Watu wanaposema "kama huna D mbili" utanielewa huwa wana maana gani?

Zamani nilikuwa naona pia humu JF watu wanakomenti sana DD kwenye nyuzi pia.
ukikosa D mbili una ziro kwenye matokeo ya kidato cha nne, na ukiwa na ziro unakosa sifa za kupata cheti
 
D mbili ni minimum pass marks. Wanamaanisha kama kidato cha nne huna D mbili basi una uwezo mdogo wa kiakili hivo hakuna jambo utaelewa
Hii imetokana na matangazo ya vyuo vya kati kutaka D mbili kwa masomo yasiyo ya Dini ili kupata admission
Mwanzishaji wa hii ni Leornard na alipata D mbili Form 6..!!!

Sasa hayo maelezo yako yaelezee ki Form 6.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Mwanzishaji wa hii ni Leornard na alipata D mbili Form 6..!!!

Sasa hayo maelezo yako yaelezee ki Form 6.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Minimum point za kuingia Chuo Kikuu ilikuwa lazima uwe na atleast Point 5 kwa masomo matatu.

A -Point 5
B-Point 4
C-Point 3
D-Point 2
E-Point 1
S-0.5 Point.
F - 0 No Point.

Kwahiyo Kiform 6 D mbili means ni point 4 Ukijulisha E moja una qualify kupata chuo kwasababu utakuwa na Point 5( D mbili na E moja).
 
yeye alisema alipata D 2 Form 6

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
D 2 maana yake ni kiwango cha ufaulu. Kwa kilaza ukipata D 2 umefaulu to the maximum
 
Back
Top Bottom