Mshahara mzuri unaanzia kiasi gani?

Mshahara mzuri unaanzia kiasi gani?

Hakuna mshahara unao mtosha mtu. HAta ukilipwa mshahara wa million 1 wewe kama wewe utakutosha ila ukianza
1 kufyatua watoto na kuwasomesha
2 kumuhudumia wife
3 kulipa ada , bill za maji umeme bima ya afya chakula usafiri
4 na ukute ndugu kijijini wanakutegemea hio pesa ni ndogo hata ulipwe million 10

Ni ishu ya wewe kujichakata uwe na mishemishe nyingi za kukuongezea kipato ili uwe na Financial Freedom
 
Mshahara mzuri ni a relative concept inayotegemea mambo mengi sana ikiwemo malengo yako. Mimi nitakuambia kuanzia laki tatu poa maana sina malengo yoyote, ila kuna mwingine humu atasema milioni 10 kwa sababu ana mipango mingi
Tuangalie kwenye engo ya kufanya maendeleo kumudu kuishi at least middle class life, kumiliki nyumba mjini na usafiri na kuanzisha mradi wa kitega uchumi hata kimoja, je ni kiwango gani cha mshahara kwa hali ya maisha ya bongo kinaweza kutosheleza?
 
Mshahara mzuri uwe na uwezo ya kulipa kodi angalau ya miezi 8 kwenye Nyumba unayoisgi. Huo ndio mshahara mzuri kwa ajili yako kama umekodi
 
Mshahara mzuri ni ule unaoendana na effort yako katika utafutaji, Uwe halali na pia uweze kukidhi mahitaji yako ya muhimu na ukabaki na akiba kwaajili ya kesho.
 
Tuangalie kwenye engo ya kufanya maendeleo kumudu kuishi at least middle class life, kumiliki nyumba mjini na usafiri na kuanzisha mradi wa kitega uchumi hata kimoja, je ni kiwango gani cha mshahara kwa hali ya maisha ya bongo kinaweza kutosheleza?
Labda tuanzie hapa
1000016867.jpg
 
Kibongobongo mshahara mzuri take home ni 1m mpaka 4.5m

Mshahara mzuri sana ni kuanzia 5m mpaka 10m

Mshahara wa kiboss/kikurugenzi ni kuanzia 10m mpaka 35m

Mshahara wa watu wazito ni kwa USD $ hasa wanaofanya kazi kwenye mashirika ya kimataifa mishahara yao huanzia $15,000 hadi $50,000+
Kuna wengine wanapata $100,000+
 
Back
Top Bottom