Kimsingi mfuko uwa unaangalia ile mishahara mikubwa zaidi ya miezi 36 (miaka mitatu) ambayo mwanachama alipokea ndani ya miaka kumi ya mwisho wa utumishi wake kabla hajastaafu. Hiyo mishahara mikubwa zaidi ya miezi 36 ndiyo ujumlishwa kwa pamoja na kisha kugawia tatu (yaani miaka mitatu) ili kupata wastani wa kipato hicho kwa mwaka mmoja mzima. Hiyo ndiyo APE kwenye formula Iliyotolewa na mdau kwenye comments za awali. Pia mfuko uangalia idadi ya miezi mwanachama aliyochangia kwenye mfuko (ambayo kwenye formula ndiyo N). Hivi vitu viwili ndivyo ubadilika kwenye formula kutegemea mwanachama na mwanachama wakati vingine havibadiliki.
Hivyo formula ya kupata kiasi cha mkupuo kusomeka kama ifuatavyo:
Commutted Pension Gratuity= (1/580) x N x APE x 12.5 x 33%.
Au kama hautaki kuangaika na mahesabu marefu tumia formula hii kupata pesa ya mkupuo:
0.007112 x N x APE.
Na formula ya kupata pension ya kila mwezi formula ni hii hapa chini:
(1/580) x N x APE x 1/12 x 67% au kwa kifupi chukua 0.0000963 × N x APE.
Kwa kutumia mshahara wa 2,116,000 na idadi ya miaka 32 (miezi 384) aliyotoa mleta mada hesabu inakuwa hivi:
Mkupuo: (1/580) x 384 x [(2,116,000 x 12 x 3)/3] x 12.5 x 0.33= TZS 69,346,427.60.