UFAFANUZI.
1/Mishahara ya watumishi wa serikali kuu ni sawa sawa na serikali za mitaa (Halmashauri). Scale zao za mishahara ni zile zile.
2/Mishahara ya watumishi wa umma kwenye mashirika ya serikali(Mashirika ya umma) ni tofauti na wale wa serikalini(yaani halmashauri au serikali kuu).
3/Sina uhakika sana na Exact figure lakini mshahara wa Engineer(Degree holder) anaoanza nao serikalini ni kama laki tisa na kitu(Bila makato), ila anapokatwa makato anabakia(Take home) na wastani wa Laki sita.
4/Katika ajira za serikalini, kada yenye mishahara wa juu zaidi ni kada ya Afya(Ambapo Daktari aliyeajiriwa anaanza na mshahara wa 1.4M kabla ya makato, na akikatwa makato anabakia na wastani wa 850,000/=) Kada zingine kama Elimu, Kilimo, Uhandisi, Uhasibu nk. hazitofautiani sana ni nadra kukuta mfanyakazi wa kada hizo anaajiriwa na kuanza na mshahara unaozidi Milioni.
5/Kwa sasa(Toka Magufuli aingie madarakani) posho mbalimbali nje ya mshahara kwa watumishi wa serikali wa kada zote kwa zaidi ya 90% hazipo kabisa(Ni kama zimefutwa kinyemela). Sio Daktari, sio Engineer nk. wote wanalia njaa.