Mshahara wa nyota mpya wa Simba, Adam Salamba ni milioni 48

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Hakuna kinachoshindikana mbele ya pesa hasa katika soka kwani imefahamika kwamba mshambuliaji mpya wa Simba Adam Salamba atavuna kiasi cha pesa ambacho hakika hakuwahi kuvuna katika maisha yake ya soka.

Inaelezwa kuwa dau la kuipata saini ya mshambuliaji huyo kutoka Lipuli limewagharimu Simba kiasi cha shilingi milioni 40 ambapo katika pesa hiyo Lipuli wamelamba milioni 25 kama gharama ya kuvunja mkataba huku Salamba akitia kibindoni milioni 15 kama ada yake ya usajili.

Pamoja na hayo, Salamba atapokea kiasi cha shilingi milioni mbili kwa mwezi katika kipindi chote cha mkataba wake wa miaka miwili ambapo jumla yake ni milioni 48 kwa kipindi chote.
 
Milioni mbili kwa mwezi sio mbaya kwa mchezaji anayejitambua anataka nini mbeleni. tafuta signing fee ya mlipili na kichuya na mishahara yao kwa mwezi halafu angalia watakapokuja kuongeza mkataba watalipwa nini. cha msingi afanye kazi ndani ya msimu huu wa ligi aongeze thamani yake simba wenyewe watapanda dau la mshahara na ada ya usajili achilia vilabu vingine.
 
Siku Yanga na Simba zitakapobeba vikombe cha Afrika nitaona wanachofanya ni cha maana Lkn hii ni ubabaishaji tu
 
Kichwa cha habari na habari kamili vipo tofauti ila umeeleweka na kila la kheri Salamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…