Mshahara wa Rais Magufuli wawa gumzo Kenya

Mshahara wa Rais Magufuli wawa gumzo Kenya

Wakenya bwana kama vipi waje tubadilishane wakae nae wiki tu waone moto wake
 
ila wabongo wengi mmevamia huu uzi wa watu.lugha imewapitia pembeni.mmejiabisha sana na kuprove ni vichwa vitupu.
wenzenu wamejaa hoja..nyie mmejaa mihemko!
aibu tupu
 
ila wabongo wengi mmevamia huu uzi wa watu.lugha imewapitia pembeni.mmejiabisha sana na kuprove ni vichwa vitupu.
wenzenu wamejaa hoja..nyie mmejaa mihemko!
aibu tupu
Ni kweli dada ulichokisema, kuna watu wameingia kichwa kichwa..
 
jamani huu Uzi upelekeni kule majukwaa mengine.

huku ni only heavy metal discussions.
maana nimeona jukwaa limevamiwa na wageni watupu ambao are not belonging to This sub forum for East Africa.
Upelekwe wapi Elia? Lol!
 
Inamaana wabunge wanamshahara mkubwa kuliko mkulu!?
Mawaziri wanamshahara mkubwa kuliko mkulu!?
Waziri Mkuu kampita mshahara aliyemteuwa!?
This is another kind of joking!!!!?

Labda alikuwa anamaanisha mshahara wa mwenyekiti wa ccm
Kwahiyo ulitaka ataje ngapi?
 
Panaitwaje?

weee tembelea tu huko kwenye majukwaa mengine utaona tu. utakuta mtu anapinga kila kitu anachosema na anachofanya rais. lkn kwa akili yangu nafikiri ni wale majeruhi wa udhibiti wa mambo kama vile;
1. udhibiti wa biashara ya madawa ya kulevya
2. udhibiti wa biashara ya pembe za ndovu
3. udhibiti wa wizi wa makasha bandarini
4. udhibiti wa kukwepa kodi
5. udhibiti wa wafanyakazi hewa
waliokuwa wanufaika wa hayo hapo juu hawawezi kumpenda rais hata kidogo. wenyewe ni kupinga tu.
lkn ushauri wa bure ni kuwa mambo yamebadirika nao wabadirike. vinginevyo watasikilizia maumivu.
 
weee tembelea tu huko kwenye majukwaa mengine utaona tu. utakuta mtu anapinga kila kitu anachosema na anachofanya rais. lkn kwa akili yangu nafikiri ni wale majeruhi wa udhibiti wa mambo kama vile;
1. udhibiti wa biashara ya madawa ya kulevya
2. udhibiti wa biashara ya pembe za ndovu
3. udhibiti wa wizi wa makasha bandarini
4. udhibiti wa kukwepa kodi
5. udhibiti wa wafanyakazi news
waliokuwa wanufaika wa hayo hapo juu hawawezi kumpenda rais hata kidogo. wenyewe ni kupinga tu.
lkn ushauri wa bure ni kuwa mambo yamebadirika nao wabadirike. vinginevyo watasikilizia maumivu.
Hilo ni kweli mkuu, nakuunga mkono, wapinga kila kitu wapo, yani hadi huwa inakera
 
The fact that it is not publicly known how much he earns makes me more worried, his public pronouncement is a distraction
 
Mshahara wa Magufuli mdogo kuliko marais wenzake
Rais wa Tanzania John Magufuli amefichua kuwa anapokea mshahara wa shilingi milioni 9 za Kitanzania kwa mwezi, sawa na dola 4000, hivyo kumfanya miongoni mwa viongozi wachache wa Afrika wanaopokea mishahara midogo.
Rais Magufuli yuko katika harakati za kufanikisha sera ambayo imeshutumiwa vikali ya kupunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya fedha za umma. Katika hotuba aliyoitoa mjini Dar Es Salam siku ya Jumanne wiki hii, Kiongozi huyo wa Tanzania alisema serikali imepunguza mishahara ya maafisa wakuu watendaji wa mashirika ya serikali hadi shilingi milioni 15 ambazo ni sawa na dola 6,700 kiasi ambacho ni cha juu kuliko mshahara wake.

Magufuli alisema kama wanahisi kiwango hicho cha fedha ni kidogo, wana uhuru wa kuziacha kazi zao akiongeza kuwa matumizi mabaya ya fedha za umma yamekithiri katika mashirika ya serikali na amekataa maombi kutoka kwa baadhi ya maafisa kuongeza marupurupu yao akihoji hawezi kuongeza mishahara ya watumishi wa umma wakati raia wa kawaida hawana huduma za maji, afya na umeme.

Tangu kuchukua madaraka mwezi Novemba mwaka 2015, Magufuli ajulikanaye kwa jina maarufu la Tinga Tinga, amepunguza matumizi ya serikali kwa kuchukua hatua kadhaa kama kudhibiti safari za nje za maafisa wa serikali, kuondolewa kwa wafanyakazi hewa kutoka kwa utumishi wa umma.

Zuma apokea Dola za Kimarekani 20,000

Baadhi ya wakosoaji wake wanamshutumu kuwa baadhi ya hatua zake zimevuka mipaka wakihoji zitaathiri ukuaji wa kiuchumi wa taifa hilo la pili kwa nguvu za kiuchumi katika kanda ya Afrika Mashariki na baadhi ya maamuzi yake yanaoekana kurudisha nyuma uwekezaji katika sekta muhimu kama madini

mshahara wa Magufuli ukilinganishwa na wa viongozi wengine wa Afrika ni mdogo mno. Kiongozi huyo wa Tanzania hana vyanzo vingine vya kujipatia kipato vinavyojulikana na serikali yake mwaka jana ilisema ina mipango ya kuwasilisha mswada bungeni utakaowazuia viongozii wa umma kujishughulisha na biashara ili kuepusha mgongano wa maslahi.

Rais wa nchi jirani ya Kenya Uhuru Kenyatta anapokea mshahara wa takriban dola 14,000 kwa mwezi, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma analipwa mshahara wa dola 20,000 kwa mwezi kufuatia bunge mwaka 2015 kuidhinisha nyongeza ya mshahara wa rais.

Kiongozi mwingine wa Afrika ambaye ana mshahara wa wastani ni Rais wa Nigeria Muhamadu Buhari ambaye alikubali mshahara wake upunguzwe kwa asilimia 50 alipoingia madarakani mwezi Mei mwaka 2015. Awali mshahara wa Rais wa Nigeria ulikuwa naira milioni 14.1 ambazo zilikuwa ni sawa na dola 70,000 wakati huo.

Mwandishi: Caro Robi/Reuters

Mhariri: Iddi Ssessanga
 
6tag-1515006017-1619493759518777894_1515006017.jpg
 
Huo ni uongo mshahara wake ni zaidi ya 35 miilioni kwa mwezi au zaidi ya milioni 400 kwa mwaka. Huyu muongo anajulikana kwa uongo wake uliokithiri. Kipi kinachomshinda kuweka salary slip yake aliyoahidi hadharani? Acheni kumuamini huyu muongo wa kiwango cha Phd. Mshahara wake ni $192,000 kwa mwaka au sawa na $16,000 kwa mwezi times 2,200 sawa na 35.2 million kwa mwezi.

Below is a brief summary of 30 highest earning African Presidents:



Country Net pay per anum President
1 Cameroon US$610,000 Paul Biya
2 Morocco US$480,000 King Mohammed VI
3 South Africa US$272,000 Jacob Zuma
4 Tanzania US$192,000 Jakaya Kikwete
5 Algeria US$164,000 Abdel Aziz Bouteflika
6 Equatorial Guinea US$150,000 Theodore Nguema
7 Kenya US$132,000 Uhuru Kenyatta
8 Somalia US$120,000 Hassan Sheikh Mohamoud
9 Comoros US$115,000 Ikililou Dhoinine
10 Congo Republic US$110,000 Denis Sassou Nguesso
11 Namibia US$110,000 Hage Geingob
12 Zimbabwe US$108,000 Robert Mugabe
13 Mauritius US$104,838 Ameenah Gurib
14 Cote D’Ivoire US$100,000 Alassane Ouattara
15 Liberia US$90,000 Ellen Johnson Sirleaf
16 Rwanda US$85,000 Paul Kagame
17 Angola US$81,075 José Eduardo dos Santos
18 Ghana US$76,000 John Dramani Mahama
19 Malawi US$75,348 Peter Mutharika
20 Egypt US$72,000 Abdel Fattah el-Sisi
21 Nigeria US$70,000 Muhammadu Buhari
22 Mali US$69,609 Ibrahim Boubacar Keïta
23 Botswana US$66,713 Ian Khama
24 Gabon US$65,000 Ali Bongo Ondimba
25 Zambia US$56,000 Edgar Lungu
26 Dr.Congo US$52,97 Joseph Kabila
27 Swaziland US$52,128 Mswati III
28 Mozambique US$47,500 Filipe Nyusi
29 Ethiopia US$44,472 Mulatu Teshome
30 Lesotho US$36,000 Letsie III
We mshenzi wanasema kashusha
 
Back
Top Bottom