Mshamba mimi sijawahi kwenda Club/disco, washamba wenzangu tukutane hapa!

Mshamba mimi sijawahi kwenda Club/disco, washamba wenzangu tukutane hapa!

Aiseee kusema kweli hii ishu ilinishinda kabisa japo masela waliniona kama niko primitive

Yani natoa hela yangu mfukoni halafu dj anapiga mziki anaoutaka yeye halafu mimi niucheze??
 
Daaaah mzee umepiga mulemule yaani mi mwenyewe hapa napenda music ya kila aina na napenda na nafanya djng kinoma lakini kwenye simple party tu kama mahafali kitchen party na HBD lakini tangu nizaliwe sijui disco la umma kabisa, club wala baa. mbaya zaidi sijawahi hata kufikiria kuwa nahitajika kwenda huko hata kujuta kuwa sijawahi kwenda disco sijawahi juta.
Wewe ni DJ?
 
Aisee sitokuja kwenda club

Siku za jumamosi,
Huwa Nawasha mziki chumbani kwangu, alafu naweka zile taa za mwanga mwanga, naanza kuscratch, au naweka playlist Kisha nachezaa wee peke yangu, nikichoka Naenda kuoga, nalala
Mtu akinifuma nahisi itakua aibu ya mwaka

Ukizaliwa Introvert ni shida aisee.
 
Kusema ukweli tangu nazaliwa sijui kitu inaitwa club au disco naskiaga tu hii kitu ila binafsi sijawahi

kabisa kwenda disco nikajua kupoje au huwa kunakuaje,ninachokumbuka nikiwa shule moro kuna

Shule yetu ilikua ni ya boys tupu (st fransis) ila pembeni ya shule yetu mtaa huo huo kuna shule ingine

ya wasichana tupu (st ann) hizi shule zote mbili ni za wakatoliki huwa kinachofanyika kwa shule hizi

kila mwezi huwa kunakuaga na disco shuleni kwetu wanachukuliwa Girls kutoka st ann wanaletwa St francis

kunakua na disco na mziki mmoja hatari sana,tuna HALL letu moja MULTPURPOSE hilo HALL ni hatari kabisa

tuna mixika humo ndani ni bang bang bang jioni vitoto vya st ann vinarudi shuleni kwao.

Sisi BOYS tunaanza maisha mapya ya story na kusimuliana disco lilikuaje...zaidi ya hapo sijawahi jua Disco huko kwingine kunakuaje

hadi leo sijawahi tamani kwenda huko disco/club japokua sijaenda na hivi nikiskia wanasema disco soda ndani inauzwa 2000 ndio kabisaaaa

wananipa sababu ya kutokwenda maana najua siwezi kwenda peke angu bila mtu pembeni,sasa kama soda ni 2000 na naskia hamna soda za chupa

aaaaaah jamani vingine mtanisimulia huwa vikoje
Sio kitu chalazima mfano: kwetu ni mm peke yangu ndio nimeenda disco, clubs nishaudhuria na matamasha kibao lakini nina kaka zangu wa 4 hawajawahi kwenda huko hata siku moja.
 
O level nilisoma shule ya dini, A level nikapiga shule ya serikali. Chuo sasa huko ndo ilikua ni patashika. Club kuanzia La Liga, Pub alberto, black diamond, baaadae wakatuletea kitu hatari sana RedStone zote mimi nazurura tu. Sema baada ya chuo nikaacha hayo mambo mimi sio mnywaji wa pombe so ilifika muda nikaona club ni kelele tu.
 
Aisee sitokuja kwenda club

Siku za jumamosi,
Huwa Nawasha mziki chumbani kwangu, alafu naweka zile taa za mwanga mwanga, naanza kuscratch, au naweka playlist Kisha nachezaa wee peke yangu, nikichoka Naenda kuoga, nalala
Mtu akinifuma nahisi itakua aibu ya mwaka

Ukizaliwa Introvert ni shida aisee.
Sema tu hujaamua kwenda, mbona sisi ma introvert tunaendaga sema sisi hatuendagi dance floor tunakaa zetu counter.
Nakumbuka wakati tupo chuo kuna jamaa yetu alikuwa na umbo la kifather father hivi yeye alikuwa akiingia club anaenda kukaa zake counter, akiwa hapo counter watoto wanamfuata hapo na kuanza kumkatikia, jamaa anawadanganya ni officer wa wizara fulani kumbe ni mwanachuo anayetegemea boom
 
Aisee, yani nikichanganyika na watu tofauti na ninaowajua au niliowazoea nakosa amani kabisa, na zile kelele huwa nahisi kuchanganyikiwa aisee.
 
Mimi sio mpenzi wa taarabu lakini kipindi kile mzee Yusuph yupo kwenye form nilikuwa sikosagi kwenye show zake, mtu unazungushiwa nyonga mpaka unatamani upige bao hapo hapo mamaeeeee.
Wengine mizuka ikiwapanda walikuwa wanapandisha madera na visketi vyao juu wanaacha vichupi tu
 
Nyie ndio wazazi siku ya harusi ya mtoto wenu unaombwa kufungua mziki DJ akiangalia umri wako anajua uyu nikimtupa kwenye I need girl ya puff dad mzee atakumbuka enzi zake

Mungu wangu yani ndani ya dakika tat unaanza kupiga msamba, push up, sarakasi, step za kwaya na viduku juu 😀😀😀

Wageni walikuwa utasikia wewe toa toa toa maana baba kawa kituko😀😀😀
 
O level nilisoma shule ya dini, A level nikapiga shule ya serikali. Chuo sasa huko ndo ilikua ni patashika. Club kuanzia La Liga, Pub alberto, black diamond, baaadae wakatuletea kitu hatari sana RedStone zote mimi nazurura tu. Sema baada ya chuo nikaacha hayo mambo mimi sio mnywaji wa pombe so ilifika muda nikaona club ni kelele tu.
Bila shaka we ni member wa Muccobs 🤣🤣🤣
 
Sema tu hujaamua kwenda, mbona sisi ma introvert tunaendaga sema sisi hatuendagi dance floor tunakaa zetu counter.
Nakumbuka wakati tupo chuo kuna jamaa yetu alikuwa na umbo la kifather father hivi yeye alikuwa akiingia club anaenda kukaa zake counter, akiwa hapo counter watoto wanamfuata hapo na kuanza kumkatikia, jamaa anawadanganya ni officer wa wizara fulani kumbe ni mwanachuo anayetegemea boom
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Me pia ukiacha ile wanaita disco toto tuliyokua tunaenda kipindi kile cha sikukuu, sijawahi kwenda disco kabisa. Sometimes naona aibu nikikutana na watu huku dar wananiuliza kuhusu club za kwetu Tanga, me sina hata moja maana hizo La Casa chika, sijui Meridian, sijui Pweza me nazipita nje tu wala sijui ndani kukoje
Mimi pia nimekulia Ta, sijawahi kuingia ukumbi wowote, nilikuwa nikiishi maeneo ya kati pale karibu na Majestic, nilikuwa nilisikia mfumo wa muziki wa club ya Twiga/la casa choke/four ways n.k. ila hata mara moja sijawahi kujisikia kwenda.
 
Back
Top Bottom