Mshamba mimi sijawahi kwenda Club/disco, washamba wenzangu tukutane hapa!

Aiseee kusema kweli hii ishu ilinishinda kabisa japo masela waliniona kama niko primitive

Yani natoa hela yangu mfukoni halafu dj anapiga mziki anaoutaka yeye halafu mimi niucheze??
 
Wewe ni DJ?
 
Aisee sitokuja kwenda club

Siku za jumamosi,
Huwa Nawasha mziki chumbani kwangu, alafu naweka zile taa za mwanga mwanga, naanza kuscratch, au naweka playlist Kisha nachezaa wee peke yangu, nikichoka Naenda kuoga, nalala
Mtu akinifuma nahisi itakua aibu ya mwaka

Ukizaliwa Introvert ni shida aisee.
 
Sio kitu chalazima mfano: kwetu ni mm peke yangu ndio nimeenda disco, clubs nishaudhuria na matamasha kibao lakini nina kaka zangu wa 4 hawajawahi kwenda huko hata siku moja.
 
O level nilisoma shule ya dini, A level nikapiga shule ya serikali. Chuo sasa huko ndo ilikua ni patashika. Club kuanzia La Liga, Pub alberto, black diamond, baaadae wakatuletea kitu hatari sana RedStone zote mimi nazurura tu. Sema baada ya chuo nikaacha hayo mambo mimi sio mnywaji wa pombe so ilifika muda nikaona club ni kelele tu.
 
Sema tu hujaamua kwenda, mbona sisi ma introvert tunaendaga sema sisi hatuendagi dance floor tunakaa zetu counter.
Nakumbuka wakati tupo chuo kuna jamaa yetu alikuwa na umbo la kifather father hivi yeye alikuwa akiingia club anaenda kukaa zake counter, akiwa hapo counter watoto wanamfuata hapo na kuanza kumkatikia, jamaa anawadanganya ni officer wa wizara fulani kumbe ni mwanachuo anayetegemea boom
 
Aisee, yani nikichanganyika na watu tofauti na ninaowajua au niliowazoea nakosa amani kabisa, na zile kelele huwa nahisi kuchanganyikiwa aisee.
 
Mimi sio mpenzi wa taarabu lakini kipindi kile mzee Yusuph yupo kwenye form nilikuwa sikosagi kwenye show zake, mtu unazungushiwa nyonga mpaka unatamani upige bao hapo hapo mamaeeeee.
Wengine mizuka ikiwapanda walikuwa wanapandisha madera na visketi vyao juu wanaacha vichupi tu
 
Nyie ndio wazazi siku ya harusi ya mtoto wenu unaombwa kufungua mziki DJ akiangalia umri wako anajua uyu nikimtupa kwenye I need girl ya puff dad mzee atakumbuka enzi zake

Mungu wangu yani ndani ya dakika tat unaanza kupiga msamba, push up, sarakasi, step za kwaya na viduku juu πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Wageni walikuwa utasikia wewe toa toa toa maana baba kawa kitukoπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Bila shaka we ni member wa Muccobs 🀣🀣🀣
 
🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
Mimi pia nimekulia Ta, sijawahi kuingia ukumbi wowote, nilikuwa nikiishi maeneo ya kati pale karibu na Majestic, nilikuwa nilisikia mfumo wa muziki wa club ya Twiga/la casa choke/four ways n.k. ila hata mara moja sijawahi kujisikia kwenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…