Mshambuliaji mpya Yanga SC Hafidh Kounkon: Nachukia Klabu ambazo zinapenda Kuroga na Uchawi

Mshambuliaji mpya Yanga SC Hafidh Kounkon: Nachukia Klabu ambazo zinapenda Kuroga na Uchawi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
"Mimi ni Mtu wa Imani (Dini) sana na sipendi tabia ya Vilabu vingi vya Afrika kupenda Kuroga na Kuamini Uchawi na nikiwa katika Timu yenye huu Utamaduni nitawakatalia na ikiwezekana hata kuomba Kuondoka" amesema Mshambuliaji mpya wa Yanga SC Hafidh Kounkon kupitia Kipindi cha Spoti Leo cha Radio One muda si mrsfu.

Tafadhali aliye karibu na huyu Mchezaji amwambie kuwa GENTAMYCINE wa JamiiForums namwambia hapo alipo sasa Kuroga na kupenda Ushirikina ni Moja ya Tunu yao Kuu na iliyotukuka hivyo ajiandae kuwa anachanjwa Ugokoni, Ulimini na Kisiginoni kila akiwa anacheza huku Jezi yake ikishoneshewa Hirizi ya Kipekee.

Yaani kabisaaaaa Timu ina Marafiki zangu Wakubwa na Wanaojua Kona zote za Waganga wa Kienyeji Tanzania nzima hadi Kisiwani Zanzibar akina Mohammed Bhinda na Said Motisha halafu isiwe Inaroga hata Mechi za Kirafiki.
 
Aje SIMBA SC sisi haturogi ila tunawasha moto tu katikati ya uwanja,soka hili hili la Africa utaomba kuondoka kwenye timu ngapi sasa hadi daraja la nne huko wanaroga...sisi tutaingia kilingeni alafu tumuache hotelini alafu uone kama atafikisha pasaka kabla hajaondoka....AFRICA,
OUR CONTINENT
OUR FOOTBALL
 
Wizard Crew kamati ya fitna kamati ya roho mbaya lazima azikwe Ng'ombe mzima mzima tukikosa Ng'ombe tunazika Ngamia wale wameenda kuwanga mlimani
 
Aanze kufungasha mabegi, maana Yanga akikutana na Simba ataambiwa achague moja kati ya mawili; ashiriki kutumia mlango usio rasmi au arudi Ghana
 
Tushampoteza huyo. Ukisikia mbuzi kafia kwa mpika supu ndiyo hii sasa
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa mtu mfanya biashara anajua gharama ya kuchafua brand ya mtu mwingine kwa sababu anayofikiri ni ya kishabiki. Posti yako haina tofauti na wale wanaoposti kuwa, mabasi ya kampuni flani hayafai, eti kwa sababu basi moja liliharibi njiani au pengine chupa za maji flani hayafai kwa kuwa alikuta mfuniko haujakaza vizuri nknk
Kwa posti inayohusu biashara ya kuingiza kipato; kabla hujaposti chochote kibaya, nivizuri ujiulize kuwa; unataka upate matokeo gani, yana umuhimu gani, yana adhari gani kwa mwenye biashara, yatakusaidia ninink nk nk
Nafikiri Ushabiki usitufanye tukaacha kutumia akili zetu vizuri......
 
Huyo Mohamed Bhinda mchawi sana, halafu Simba ikicheza unamuona anakaa karibu na viongozi wa Simba kusikiliza umbea.
 
Kwa mtu mfanya biashara anajua gharama ya kuchafua brand ya mtu mwingine kwa sababu anayofikiri ni ya kishabiki. Posti yako haina tofauti na wale wanaoposti kuwa, mabasi ya kampuni flani hayafai, eti kwa sababu basi moja liliharibi njiani au pengine chupa za maji flani hayafai kwa kuwa alikuta mfuniko haujakaza vizuri nknk
Kwa posti inayohusu biashara ya kuingiza kipato; kabla hujaposti chochote kibaya, nivizuri ujiulize kuwa; unataka upate matokeo gani, yana umuhimu gani, yana adhari gani kwa mwenye biashara, yatakusaidia ninink nk nk
Nafikiri Ushabiki usitufanye tukaacha kutumia akili zetu vizuri......
Urewedi mkuu?Ja mithi...chamkera mghenji,vyothe viringane...[emoji1787][emoji1787]
 
Kama ndio misimamo yake basi krismas atakula kwao maana hapo alipo ndio uchawini kwenyewe.
 
Back
Top Bottom