Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Mshambuliaji wa Liverpool, Diogo Jota, ameripotiwa kufariki dunia katika ajali ya gari huko Uhispania akiwa na umri wa miaka 28, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Ureno.
Inaripotiwa kuwa Jota alikuwa akisafiri ndani ya gari pamoja na kaka yake Andre, ambaye naye ni mchezaji wa mpira wa miguu mwenye umri wa miaka 26,ambapo mara baada ya ajali kutokea gari liliwaka moto.
Tukio hilo limetokea katika barabara ya A-52 katika jimbo la Zamora, Uhispania.
Jota ambaye amepoteza maisha siku 10 tu tangu afunge ndoa na mpenzi wake Rute Cardoso mnamo Juni 22, 2025 huku akiacha watoto watatu.
Nyota huyo wa zamani wa Wolverhampton amehudumu Liverpool kwa miaka mitano akiichezea timu hiyo mechi 123 na kufunga magoli 47. Pia ameichezea Ureno mechi 49 na kuifungia magoli 14