Mshamu (Mtoto wa Jangala) yuko wapi sasa hivi na jina lake halisi

Fao La Kujitoa

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2016
Posts
396
Reaction score
966
Vijana wa zamani kama mnakumbuka miaka ya mwishoni 80. Kulikuwa na mchezo wa kuigiza wa redio RTD kila jumapili usiku yani watu hawakosi ikifika tu saa mbili usiku jumapili watu wameshajikusanya karibu na redio.

Mchezo huo ulikuwa unadhaminiwa na kibuku. Mzee Jangala alikuwa maarufu sana na kijana wake Mshamu. Kuna episode flani ilibamba sana hadi kesho yake jumatatu ikawa gumzo kila mahali mitaani. Mshamu alivyomvamia baba yake Jangala kalewa na masela wake na kumpiga na kumuibia hadi Jangala akamlaani huku akikimbia. Marafiki zake Mshamu wakawa wanamcheka na kusema huu msemo "Acha masikhara wewe dingi lake mshamu anayeya kama pajero".

Huyu mshamu yuko wapi siku Hizi na jina lake kamili?

Wanajamvi jukwaa lenu
 
Mshamu kama kumbukumbu zangu ni nzuri alikuwa anakigugumizi flani wakati akiongea, nilikuwa napenda kumsikia akiongea
 
Mshamu kama kumbukumbu zangu ni nzuri alikuwa anakigugumizi flani wakati akiongea, nilikuwa napenda kumsikia akiongea
Kiatu ndio alikua na kigugumizi. Pia kulikua na Tomato. Hawa walikuja kuhitimisha uwepo wa ile michezo ya radio ya kina mzee Hamis Tajiri(Majengo), Ibrahim Raha (Mzee Pwagu), Ally Keto(Pwaguzi), Tunu Mrisho(Mama Haambiliki), Zena Dilip, Rajab Hatia(Mzee Kipara), nk
 
Majina yao ya kuigiza mazuri aisee
 
Na bado najiuliza lini tutaacha huu mfumo wa sanaa ya uigizaji. Bado tunautumia mfumo huu huu wa audio.
Leo hii kama unatizama bongo movies mtu asipo sema wamenipiga kweri na wameninyang'anywa kila kitu huwezi jua kama kuna mtu kapigwa sana na kunyang'anywa kila kitu. Bado hatujabadilika
 
Ule wimbo ulikuwa unaimbwa

Kibuku oyeeee
Hongera, hongera, hongera
Kibuku oyeeeeee
Hongeraaaaaaaaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…