Mshamu (Mtoto wa Jangala) yuko wapi sasa hivi na jina lake halisi

Mshamu (Mtoto wa Jangala) yuko wapi sasa hivi na jina lake halisi

Vijana wa zamani kama mnakumbuka miaka ya mwishoni 80. Kulikuwa na mchezo wa kuigiza wa redio RTD kila jumapili usiku yani watu hawakosi ikifika tu saa mbili usiku jumapili watu wameshajikusanya karibu na redio.

Mchezo huo ulikuwa unadhaminiwa na kibuku. Mzee Jangala alikuwa maarufu sana na kijana wake Mshamu. Kuna episode flani ilibamba sana hadi kesho yake jumatatu ikawa gumzo kila mahali mitaani. Mshamu alivyomvamia baba yake Jangala kalewa na masela wake na kumpiga na kumuibia hadi Jangala akamlaani huku akikimbia. Marafiki zake Mshamu wakawa wanamcheka na kusema huu msemo "Acha masikhara wewe dingi lake mshamu anayeya kama pajero".

Huyu mshamu yuko wapi siku Hizi na jina lake kamili?

Wanajamvi jukwaa lenu
Nakunbuka uke mchezo wa Redio ulikua unahusu utunzaji wa Mazingira. Dili zote za Mzee Jangala zilimua against Mazingira. Tukio la mwisho ni alipoanzisha project ya kukata mbao za mikoko
 
Back
Top Bottom