Mshana Jr, agent wa Shetani JF?

Mshana Jr, agent wa Shetani JF?

Haya ndo Matatizo ya kukaririshwa vitu toka mdogo badala ya kujifunza na kuelewa
 
Akitumia elimu yake aliyoipata nchini Afrika kusini ya Budhisim...na mchanganyo wa vitabu mbalimbali vya kishetani...ujuzi wake katika meditation na ulozi...

Sasa amekua kinara katika mada zote za kishetani hapa jukwaani JF... Na kwa kuwa Jf kila mtu anavutiwa na mada hizi za kutisha na kustaajabisha...basi amepata wafuasi wengi akiwafundisha na kuwaelewesha na polepole kuwaelekeza namna ya kufanya...si tu katika meditation bali pia katika vitu hatari kama viapo vya damu,uzuri wa shetani,eti lucifer sio shetani...na mengine mengi ambayo amekua akiyatoa....

1) Kuweni makini na anayoyasema
2) Na muwaze na kuamua ni kwa faida ya nani mnajifunza haya
3) Mkajiulize je Mungu wenu anafurahia hayo?
4) Na kwann watu wengi mnaotaka sana kujua haya ni wakristu?
5) Muogopeni mno...anataka kuwapotosha imani yenu

Hayo ni maoni yangu..

mmegongana anga zipi? wewe na mwenzio?
 
nimesoma thread nzima na kila comment na page zake zote. kwakweli nimeishia kuchanganyikiwa. kichwa kinagonga na ninahitaji hedex

#mimi ni yule mwenye kuchukuliwa na kila upepo wa elimu# nipo njia panda
 
Kiukweli meditation ni ushetani....ni sawa kabisa na kuuhack mwili

Nadhani bado huna uhakika na kitu unacho kiongea.....tuthibitishie kama meditation ni ushetani...bila shaka umepaniki unaongea vitu ambavyo hujafanyia uchumguzi wala hujavijua ninini.....
 
Shetani hayupo. Sema jingine.

100% naungana na wewe kuwa hakuna kitu called shetani....katika kanuni ya jozi shetani ni kinyume cha mungu...ni sawa na kusema nuru kinyume chake ni giza.....uhai kinyume chake ni mauti/kifo....hakuna shetani bali nuru/mungu ikitoweka giza huwepo....watu wanadhani shetani ni kiumbe sio kweli....
 
maishapopote kwanza nikupongeze sana kwa kutoa dukuduku lako ikiwa ni mtazamo wako kwangu kuhusiana na mada zangu
Najua ni una mengi zaidi ya kuandika kunihusu mimi na mada zangu na mambo yote yanayohusiana nazo...nitapenda kuwa bega kwa bega nawe Katika kueleweshana na kujuzana kwa uwazi na kwa mifano stahili huku tukitumia nukuu na lugha za kistaarabu
Naomba ushirika wako wa Karibu Katika hili kwa manufaa ya jukwaa

kaka, wanasema wewe ni agent wa ibilisi? ni lucifer au ni shetani yupi unamuagentia?
 
Last edited by a moderator:
100% naungana na wewe kuwa hakuna kitu called shetani....katika kanuni ya jozi shetani ni kinyume cha mungu...ni sawa na kusema nuru kinyume chake ni giza.....uhai kinyume chake ni mauti/kifo....hakuna shetani bali nuru/mungu ikitoweka giza huwepo....watu wanadhani shetani ni kiumbe sio kweli....

Ukisema shetani hayuko unatoa tafsiri wewe ni mwabudu shetani mwenyewe, kwa kuwa ni mungu wako na si kiumbe mlaaniwa kwako.
 
Wengine tunaenda kusali ili kurefresh mind kwa vinanda na vinubi vya kanisani
 
100% naungana na wewe kuwa hakuna kitu called shetani....katika kanuni ya jozi shetani ni kinyume cha mungu...ni sawa na kusema nuru kinyume chake ni giza.....uhai kinyume chake ni mauti/kifo....hakuna shetani bali nuru/mungu ikitoweka giza huwepo....watu wanadhani shetani ni kiumbe sio kweli....

Soma masomo ya kiroho utapata ufahamu mkubwa kuhusu habari za Mungu miungu shetani ibilisi mapepo majini vibwengo vinyamkera malaika etc
 
Nadhan kama kuna kitu ambacho kinamfanya mtu kuwa mpumbavu na lofa wa kisasa....ni kule kukataa kujifunza kitu kipya...au kutokuwa tayari kuhoji misingi ya imani yako in light of available evidence...!
 
Back
Top Bottom