Mshangao: Raila Kisumu Kwa Maandalizi Ya Kumpokea Rais Uhuru

Sasa tanzania kuna nani ana ugonvi wa kisiasa? Unafananisha vitu ambavyo havipo. Nenda kajifunze yaliyotokea kenya ndio uje ulinganishe na Tz. Tanzania mabadiliko yaligeuka mafuliko kisha yakachimbiwa mtaro yakaelekezwa baharini alafu wakaja wenye akili wanaongoza nchi .
 
Tusisahau sisi tanzania pamoja na sifa zetu nyingi Dunia,moja ya sifa kubwa tanzania tuliyowai kupata ni pamoja na sifa ya upatanisho kupitia kina kambarage?
 
Hivi kupendana kati ya vyama na vyama ni kitu cha kuweza kukijengea hoja kweli?
Mbona kupendena ni amri?
 
Kenya kuna watu Tz kuna maiti zitembeazo.Ukiwezachunga ng'ombe utoshindwa kuwatawala wtz.Watu waoga,wanafiki,wabinafsi,vigeugeu,hawana umoja,
 
Wameshajifunza kutokana na matokeo ya mgawanyiko. Sasa na sisi ndio tuko darasani. Hatujawahi kujua athari za migawanyiko. Tutakapojifunza kama wao, na sisi tutabadilika na kuwa na siasa zilizostaarabika.
 
sisi haya ya kwetu hata hayana sera wala dira hayajui yanaekea wapi yao kazi kubwa ni kupinga tu

kwani mkuu anaetakiwa ku solve hili ni upinzani pekee, mbona husemi mambo wanayofanyiwa wapinzani na chama chako, unahisi nyie ndio mnataka makubaliano wakati mnawaona wapinzani ni adui.

Acha mihemuko,
 
Mkuu maneno yako ni mazuri ila case study ndio mbovu, JariBu nchi nyingine huenda wazo lako likafanikiwa
 
Juzi Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Nchi za East Africa ulivunjika...kuna member mmoja anahisi anaonewa!!! hao walioweza wanashindwaje kumshawishi huyo Jamaa?
 
Na wosia wote ule tulioachiwa na mwl,mpaka maandishi tukubali Kenya watupite kiipatanishi?
 
Sasa mtu anakupigia usiongee,halafu yeye aongee,mapatano hayo yatatoka wapi? Zamani watu walikuwa guru full kuliacha,sio Sasa vino
Nalog off
 
Tanzania na Kenya sasa hivi ni nchi mbili miles apart na wanaongozwa na viongozi wenye "Varying Characters" na pia wanaotokana na "Different Historical Backgrounds".

Hivyo yanayofanyika Kenya hayawezi kabisa kufanyika Tanzania kwa sababu hizo nilizozitaja hapo juu.

Wakati Kenya wana katiba inayotambua haki za msingi za kiraia, Tanzania tuna katiba ya viraka ambayo imenyakua mamlaka yote toka kwa wananchi na kumrundikia rais ambaye anayatumia kwa kadri anavyojisikia.
 
Hatuna haja na watetezi wa mafisadi na mabeberu furaha yao ni ndege zetu zikamatwe, dhahabu zetu ziendelee kuibiwa, tuzidi kushtakiwa mahakama za nje ili tufilisike, kupinga kila kitu hata yale waliokua wakiyapigia chapuo zamani

To hell with those people, now they are dying naturally, Tanzania yetu ya wazalendo hiyooo inapepea, huku Sgr kule Stigler's, pale ndege, huku hospitals, pale bandari, huko mibarabara na mi flyovers, hapa mapato manono, huko Airport yaani hatupoi.
 
Sio kwa CCM hii tunayoijua.

Kwanza Kenya ina watu wanaojulikana both Chama tawala na Wapinzani...sisi Tanzania tuna jamii ya Watu wasiojulikana.

Ulishawasikia hao popote tena duniani?

Utapatanaje na watu wasiojulikana?
Hahahaaaaa,just hahahahaaa.
 
Muulize Magufuli kisa cha kutaka kufuta vyama vingi kwa muswada huu wa kishamba , CCM ndani ya demokrasia ya kweli haiwezi hata kumaliza wiki 1
Mnachosha kila siku kulialia tuu na kusaka sababu za kulalamika bora awafute tu tupumzike na hizo kelele zenu
 
Magufuli ana siasa zipi za kuunganisha watu?? Embu tuweni serious kidogo ndio zile za kuwapiga vijembe wapinzani wakienda kwenye mikutano yake?? Au ndio zile za kuapa kuwa hakuna mpinzani atamshirikisha kwenye serikali yake hadi akamshangaa shein kwa kuteua mawaziri wapinzani.

Tuwe wakweli tu uhuru wa siasa kenya umezidi wa kwetu ndio maana Raila licha ya kujiapisha hakukamatwa wala kuuawa tofauti na kwetu hapa maalim seif akijaribu tu hilo anaweza chinjwa asubuhi tu.

Magufuli ajifunze kwa kenyatta kuwa na siasa za kuvumiliana maana kwa campaign za 2017 nilitegemea Uhuru angeweka bifu kubwa na NASA lakini haikuwa hivyo baada ya uchaguzi alijishusha na hadi kuwaachia wajiapishe na baadae akamalizana nao kwa amani.

NB siasa za kenya huzijui kabisa vijembe katukanwa sana stejini kabisa nakumbuka Joho,Mishi mboko kina Babu owino n.k waliwahi mtukana na kejeli za kutosha leo hii unasema hawana matusi??? Kuhusu siasa usipotoshe kenya kila siku siasa inaongelewa kuanzia misibani hadi kwenye sherehe.... Juzi tu hapa kina Oscar Sudi walimtolea povu gideon moi kugombea urais na huko pwani Kina mohammed said kutoa povu juu ya Joho siku ya dhifa za kitaifa

Then mlumumba unakuja potosha hapa ili uonekane mzalendo..... Funny
 
Shida yenu hamjui siasa za kenya mnakuja tetea msiolifahamu una uhakika wanasiasa wa kenya wa upinzani wana ustaarabu??


Hivi hili tusi angetukanwa Magufuli leo hii Babu angekuwa uraiani kweli if at all sio kaburini??

2. Kuhusu suluhisho inaonekana huna unalojua kwenye siasa....

a) Wapinzani formally wanapinga na kushauri bungeni ndio maana wanatoa maoni ya page kama 100 kwa kila hotuba ya wizara be it bajeti au muswada wa kisheria....

b)Pia wana bajeti mjadala ambako wanaweka masuluhisho yao juu ya ukosoaji waliofanya kwenye bajeti ya serikali kuu sasa kama hiyo sio suluhisho ni nini.

c)Pia kuna vitabu vya sera za vyama na ilani za uchaguzi wa upinzani huko wanaweka sera mbadala ambazo serikali kuu haijaweza kuziainisha kwa ukamilifu wake sasa kama hiyo sio suluhisho ni nini

3. Kuhusu kujibu matukio ya serikali ya CCM hyo ndio principle kazi ya upinzani yaani kucheck serikali iliyopo madarakani kwamba ikikosea tu basi ikosolewe na irekebishwe sasa kama unataka magufuli akikosea eti asiambiwe basi haina maana ya kuwepo upinzani

Naona elimu ya uraia huna umebakia kuongea irrelevance mbele ya wakenya.... Kwa hali hii tutaendelea tu kuwa LDC milele.
 
Typical Tanzanian thinking.... Eti chadema watetea mafisadi wakati list zote za wezi wa makinikia,Tegeta ESCROW,Almasi,Tanzanite n.k wametajwa CCM watupu kuanzia wabunge mpaka mawaziri je ni hatua gani zimechukuliwa mpaka leo dhidi yao??? Kma hakuna aliyechujua hatua waweza nisaidia nani hapo ndio mtetezi wa mafisadi!!

Hivi wapinzani wamepinga nini walichopigia upatu nielezee kimoja tu maana naona hii hoja mmekaririshwa tu.... Nitajie kimoja tu.
 
Sidhani kama unaelewa ulichondika,huku kwetu ni vice versa...jiwe ndo anachochea uadui..baada ya uchaguzi nakumbuka raila alijiapisha..imagine jiwe ndo angekuwa raisi kule nini kingetokea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…