Kenya wameweza kulikoni sisi tanzania?
Wakenya wameweza kumaliza tofauti zao za kisiasa na kiitikadi,na Sasa ni wamoja wanaijenga Kenya yao kwa umoja,mshikamano na amani,kwanini sisi tanzania tumeshindwa kumaliza tofauti zetu za kisiasa,kiitikadi, na mshikamano umoja,amani na upendo?
Tanzania miaka ya nyuma sisi ndio tulikuwa tunaongoza kwa mshikamano,maridhiano ya kisiasa na upatanishi katika bara la Africa na dunia,ni nini kimeikumba nchi yetu tanzania?
Kanisa katoliki,kkkt,bakwata,na jumuiya nyingine,mnajua kupendana ni amri?
Nawaomba viongozi wastaafu,makanisa,misikiti,na Kila mdau mcha mungu,tujitahidi kupatanisha pale palipo na mpasuko
Mungu ibariki tanzania na watu wake wote